Sehemu Ya Kwanza (1)
Ulikuwa usiku wa manane,ambapo katika mbuyu mkubwa kuliko yote kijijini Isegeye walikutana wachawi wakubwa kwa wadogo,ambapo katika ule mkutano walijadili jinsi gani ya kumuunganisha kijana Makongoro katika familia ya kichawi. Makongoro ambaye ni kijana mgeni hapo kijijini aliyekwenda kuwasabahi bibi na babu yake baada kuhitimu Elimu ya msingi.
Hivyo kwa kuwa ulikuwa ndio utaratibu katika hicho kijiji kuweza kumfanyia vitibwi mgeni anae ingia lada zao,ndio maana mapema sana wachawi wa kijiji hicho wakaamua kumuwekea kikao Makongoro ili wamjaribu.
Naam! kikao kilidum ndani ya masaa mawili,ambapo uliweze kupatikana mwafaka kwamba wamwache kwanza Siku mbili au tatu makongoro ayazoee kwanza mazingara ya kijiji cha hicho,Na bada ya hapo ndipo waanze kufanyia mambo yao kama walivyo zoeleka.
Siku zilisonga,wakati huo kijana Makongoro akiendelea kuyafurahi maisha ya kijijini..Haswa jinsi alivyokua akijidekeza mbele ya bibi na babu yake,pasipo kujuwa nini kitakacho mtokea siku za usoni…Na hivyo baada Makongoro kuzoeleka kijijini,hatimae Wachawi walirudia tena kujikusanya muda uleule mahali pale,sehem ambayo baadhi ya wanakijiji walikuwa wakiigopasana kukatiza hasa pindi giza liingiapo.
“Habari zenuu..wana wanzego”…Ni sauti ya mkuu wa kikao aliyosikika akiwa salimia wachawi wenzake,mara tu wote walipokuwa wametulia kwenye ule mti mkubwa kuliko yote kwa niaba ya kusikiliza kipi kitajiri baada kikao cha kwanza kumalizika bila kufanya mambo makuu kwa kijana mgeni aliyeingia kijijini kwao,nae si mwingine ni Makongoro.
Wachawi hao baada kusalimiwa na mkuu wao wa kikao,wote kwa pamoja waliitikia..Wakati huo sauti mbalimbali za ndege wa ajabu zikisikika kwa mbali,pamoja na upepo uliokuwa ukivuma polepole ili kuwasaidi kupata taarifa za hatari nao vilevile ulikuwa ukivuma. Baada kuitikia salamu hiyo,ndipo mkuu wao alipo sema.
“Nadhani kila mmoja anatambua kwamba siku kadhaa zilizopita,kuna mgeni kaingia hapa kijijini kwetu…Na sisi kama wanakijiji wa hiki kawaida yetu ni lazima tumjaribu mgeni yoyote yule aingiae kijijini kwetu..Hivyo basi..Mzee mwakipesile nakuomba ufanye hiyo kazi kwa vyovyote vile lazima yule kijana aungane na sisi..Sawaaaah”
“Sawaaaaa..Bi kileleganya” Aliitikia Mzee mwakipesile,baada mkuu wa mkutano kumteua kuifanya kazi ya kumvuta kijana makongoro ili ajiunge kwenye jamii ya kichawi,wakati huo babu yake makongoro ambaye aliitwa Mzee Baluguza,nae alikuwa ni mchawi aliye jitegemea.
Hivyo mkuu yule wa kikao kwisha kumteua mtu,hatimae waliagana kisha kila Mchawi akapotea pale chini ya ule mti ambao ulikuwa kama ukumbi wa mikitano ya wachawi.
Mara baada ya hayo kupita,hatimae kesho yake asubuhi Makongoro aliamshwa na bibi yake ili waende shamba,lakini kwa ukarimu na adabu aliyokuwa amejaliwa kijana Makongoro..Alimtaka bibi yake abaki nyumbani ili shamba aende yeye peke yake,kwani alimuonea huruma bibi yake ambaye tayali ameshakwishakula chumvi nyingi. Lakini Makongoro alipomwambia hilo suala bibi yake, alikataa kwa kudai kuwa nibora waende wote.Kitendo hicho kiliweza kuzua ubishi fulani kati ya bibi na mjukuu..Na kabla hawajapata jibu muafaka,ghafla alitokea Mzee Mwakipesile,moja kwa moja alikwenda mpaka mahali walipomesimama bibi na mjukuu waliokuwa wakiendelea kubishana.
“Habari za asubuhi jamani”..Ilikuwa ni salam ya Mzee mwakipesile,aliyoitoa mara tu alipo wafikia Makongoro na Bibi yake,kitendo ambacho kiliweza kusitisha ubishi wa Makongoro na Bibi yake.
“Bi Mazoea..Embu mwache kijana nae akajifunze maisha ya kufanya kazi peke yake bwanaa..utambania mpaka lini??Eee sio vizuri kiukweli”
Mzee mwakipesile ambae ndio aliyeteuliwa na wachawi wenzake kufanya kazi ya kumwingiza Makongoro kwenye familia ya kichawi…Alimwambia hivyo Bi mzoea ambae ndio bibi yake Makongoro,kwa sauti ya upole.
Na hapo ndipo Makongoro alipo muunga mkono Mzee mwakipesile,Bi mazoea akawa amekosa nguvu ya kumkataza Makongoro..Alimwacha aende akafanye kazi shambani huku akimtaka arudi nyumbani mapema,Makongoro alicheka kwanza kisha akasema
“Sawa mke wangu we usijali, ila niandalie ugali na mlenda maana hiyo mboga ndio inayo nifanya nipasahau mjini”
Alisema Makongoro huku akitupia na utani uliomfanya Bi mzoea kuyaanika mapengo yake nje kwa furaha ya kufurahishwa na utani wa mjukuu wake.Baada Makongoro kuondoka shambani,hatimae Mzee mwakipesile aliweza kukaa kitako na bibi yake Makongoro huku akionekana kumdadisi maswali mengi kuhusu Makongoro,kweli baadhi Bi mazoea aliyajibu lakini mengine alishindwa kwani alijua tabia ya wanakijiji hicho…lakini yote kwa yote baada ya mazungumzo,hatimae Mzee mwakipesile aliagana na bibi yake Makongoro kisha akaondoka zake..Mzee Mwakipesile alipoondoka,punde si punde Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro mume wa Bi mazoea aliingia Nyumbani kwake huku mkononi akiwa na wanyama fulani aina ya ndezi…Cha ajabu kabla hajaingia ndani Mzee Baluguza alihamaki kwa hasira kali akimuuliza mke wake ambae ndio Bi mazoea”Nataka uniambie,huyu Mzee mwakipesile kafuata nini hapa nyumbani kwangu” Bi Mazoea hakimjibu zaidi aliomba msamaha Kwa maana alishindwa kumtimua kwa sababu yeye na Mzee Mwakipesile ni kundi moja katika uchawi..Lakini Mzee Baluguza licha ya kuombwa samahani,hakutaka kuelewa na zaidi alicharuka baada kuuliza wapi alipo kwenda mjukuu Makongoro na kujibiwa kuwa kaelekea Shambani.
Kwa hakika Mzee Baluguza alizidi kuchanganyikiwa,huku akimtolea mke wake maneno makali ya kiruga alielekea chumbani kwake kuchukua kibuyu chake cha kichawi ili apate taarifa kuhusu mjukuu wake huko shambani.
Jasho la kutosha likimtoka Mzee baluguza akihofia usalama wa mjukuu wake,hatimae alichukua unga mweusi aliouchanganya na dam chache iliyokuwemo kwenye kile kibuyu…kisha akaongea maneno yake ya kiruga huku mkono wake ulioshikilia kibuyu ukiwa juu mfano wa mtu anae tafuta Network kweny simu yake…Punde si punde alitokea bundi ambae moja kwa moja alitua kwenye bega la Mzee baluguza,ambapo Mzee baluguza alimchukua yule bundi kisha akamtwaa kwenye mikono yake alafu akaongea kiluga tena..Na ghafla yule bundi aliruka akayeyukia angani,ipatayo nusu saa akawa amerejea tena moja kwa moja alitua kwenye ungo mahususi ambao Mzee baluguza alikua amesha uandaa..Wakati huo Bi mazoea nae alikuwa akiombea yule bundi alietumwa kuchukua taarifa kuhusu Makongoro aweze kuja na taarifa njema ili amalize siku kwa amani.
Hivyo baada yule bundi kutua kwenye ungo wa Mzee baluguza,haraka sana Mzee balu alimchukua kisha akamtazama machoni kwa maana yule bundi wa kichawi wa Mzee baluguza alikua akinasa taarifa kwa kutumia mboni zake..Na mala baada Mzee baluguza kumtazama mala mbilimbili yule bundi kwenye macho yake..mala ghafla.
Ghafla alishtuka huku akimtazama mke wake jicho ngebe,wakati huo Bi mazoea akiendelea kuwadaa ndezi alioletewa na mume wake ambae ndio Mzee baluguza.
Hivyo Mzee baluguza baada kushtuka,alikohoa kidogo..kikoozi ambacho kilimfanya Bi mazoea kumgeukia mume wake…Na hapo ndipo alipo kutana uso kwa uso na mume wake.
“Unamtazama nani?? lione mapengo yake sasa,pumbafu mbwa koko wewe”
Alieyaongea maneno hayo alikua ni Mzee baluguza akionekana kukasilishwa na kitu alichokiona kwenye mboni za bundi wake wa kichawi…Lakini licha ya Bi mazoea kutukanwa,ila alikaa kimya kwani tangu enzi za ujana wao alimtambua vema kuwa mume wake ni mkorofi,na ndio maana aliondolewa kwenye kundi la wachawi wa pale kijijini kwao bhonde..
Basi shambani nako,baada makongoro kufanya kazi kwa muda mrefu.Hatimae aliamua kuanza safari ya kurudi nyumbani,ambapo alikuwa yupo njiani alikutana na Mzee mwakipesile…Mzee ambae alipewa majukum na mkuu wake wa kichawi kwamba aifanye shughuli ya kumuunganisha makongoro katika familia ya kichawi.
“kijana habali yako”
Mzee mwakipesile alimsalimia Makongoro..Makongoro alishtuka baada kuskia mtu akiongelea nyuma yake,kitendo ambacho kilimfanya ageuke nyuma haraka ili kumtazama mtu aliemsalimia.
“Aah Mzee shkamoo”
“Malakhaa ujambo kijana wangu”
“mimi sijambo mzee wangu sijui wewe”
Mzee mwakipesile akitabasam,alijibu.”Haswaa mimi pia niko vizuri…eeh wapi unaelekea sasa”
“Mda huu narudi nyumbani baada kumaliza kazi” Alijibu hivyo Makongoro huku akipiga hatua polepole za kuondokea..Lakini Mzee mwakipesile alimsimamisha.
“Simama basi mjukuu wangu..au unaskia njaa kali”Mwakipesile alimuhoji Makongoro.
“Ndio babu”
“Anhaa hilo sio tatizo..Ebu twende kuleee unakoona miti mingi ya miembe ..au hupendi kula maembe?…maana nyie watoto wa mujini bhana mnamaringo sana”
Mzee mwakipesile alimwambia hivyo Makongoro huku akimaliza kwa kicheko ambacho kilimfanya Makongoro nae acheke..”Hapana babu sio wote,mfano mimi nimeyapenda sana maisha ya hapa kijijini kwenu na wala sina mpango wa kurudi mjini”
“Teh teh teh sawa kijana..pita vizuri maana njia hii imejaa miba”
Naam!story mbili tatu ziliendelea kati ya Mzee mwakipesile na Makongoro,wakati huo wakiwa njiani wakielekea shambani kula maembe.
“Khaa babu hivi miembe hii yote ya kwako?..”
Baada kufika shambani na kukuta miti mingi ya miembe iliyoivisha kwa ustadi..hatimae Makongoro alipigwa na butwaa hivyo akawa amemuuliza hivyo Mzee mwakipesile.
“Ndio mjukuu wangu,kwani huko mjini hakuna miti ya miembe?..”
Makongoro alicheka kidogo baada kuulizwa swali lile na Mzee mwakipesile kisha akajibu..
“Haah babu acha kunivunja mbavu bhana..sasa mjini utalima wapi”
“Lakini naskia huko mjini wanawake wazuri wapo wengi..eti ni kweli rafki yangu?..”
“Ndio wapo wengi tu..ila pesa yako babu”
“Mmh kwahiyo mpaka hela?..”
“Ndio babu,siunajua kizuri ghalama?!..”
“Haya mjukuu wangu ngoja ipo siku na mimi nitaenda huko mjini nikawaone hao wanawake wazuri..”
“sawa babu karibu…ingawa mimi bado nipo nipo kwanza hapa bhonde”
Hakika yalikua ni mazungumzo marefu ambayo Makongoro alikua akizungumza na Mzee mwakipesile,wakati huo wakiendelea kula maembe.
Na baada kumaliza,hatimae Mzee mwakipesile alimwonyesha njia ya kutokea Makongoro ili arudi nyumbani kwa bibi yake…Hivyo baada Makongoro kutokome,ghafla ile miti ya miembe ilegeuka kuwa wachawi ambapo walimpa hongera mzee mwakipesile kwa kujenga ukaribu na kijana makongoro huku wakizidi kumpa moyo kuwa asikate tamaa bali aendelee nae kujenga urafiki mpaka pale atakapo vutwa kwenye familia ya kichawi.
Baada ya hayo,hatimae walijumuika pamoja wale wachawi kisha wakacheza na kuimba nyimbo zao asili..wakati huo kila mmoja akipotea baada ya dakika moja mpaka pale wote walipo kwisha akawa amebaki mzee Mwakipesile ambae nae alikua akijipanga kupotea ila alistisha huo mpango baada kutokewa na Mzee baluguza babu yake makongoro.
Alishtuka mwakipesile…huku Mzee baluguza akipiga hatua kumfuata alipo kuwa amesimama…Na baada kumfikia alimwambia kwa sauti ya polepole
“Cheza na watoto wa kijiji hiki, ila usicheze na mjukuu wangu…nadhani umenielewa…la sivyo mtataka vita kati yangu na nyinyi..”
Mzee baluguza alimwambia hivyo Mzee meakipesile..wakati huo mwakipesile akihemea juju…
Na baada Mzee baluguza kusema hayo aliyeyuka..akimwacha Mzee baluguza akijitafakali mala mbilimbili jinsi gani atampata kijana makongoro hali ya kuwa babu yake ameshamchimba mkwala.
Basi hatimae usiku uliingia..ambapo mala baada kumaliza kula chakula cha usiku.Mzee baluguza alikaa kitako na mjukuu wake kisha akamwonya Makongoro kuweka mazoea na yule Mzee mwakipesile..Hivyo Mzee balu alienda mbali zaidi akimwambia kwamba endapo kama hatokua mskivu basi atamrudisha mjini kwa wazazi wake..Kitendo ambacho kilimfanya makongoro kuomba msamaha,huku akijiuliza kwanini babu yake anamkataza kuweka mazoea na yule Mzee wakati ana roho nzuli??..Lakini yote kwa yote Makongoro alitii agizo…Na hivyo siku hiyo aliamua kwenda kulala mapema kwani alikasirika.
Hivyo basi baada saa saba usiku kuingia..wakati huo Makongoro akiwa kwenye dimbwi la njozi,ghafla alishtuka kutoka usingizini baada kuskia nyimbo za asili zikiimba jirani na nyumba ya bibi yake…Apapo aliinuka kisha akaenda kufungua mlango ili ashuhudie kilichokuwa kikiendelea…
“Yesu wangu..?”
Alishtuka Makongoro baada kufungua mlango,na kushudia kundi la wachawi wakicheza kwa kuzunguka huku wakiwa uchi…ila kwa kuwa mwanga wa mbalamwezi ulikuwa hafifu,hivyo Makongoro hakuweza kuziona sehem nyeti za wale wachawi.
Basi nyimbo na vigelele za wale Wachawi ziliendelea wakati Makongoro akiendelea kuwatazama bila wao kujuwa,lakini punde si punde wale wachawi walipotea..ila alisalia mchawi mmoja tu ambae nae alipiga hatua kuja mlangoni ambapo alipokuwa Makongoro.
Basi Makongoro alipomwona yule mchawi akija mahali alipokuwa amesimama,haraka sana alifunga mlango kisha akatimkia kitandani kwake…wakati huo akiwa bado hajamjuwa vizuri yule mchawi aliekuwa akimfuata,ingawa alikuwa na mashaka kuwa huwenda akawa ni bibi yake kwani mwendo wa bibi yake na mwendo wa yule mchawi aliemwona nje,wote walifanana…Lakini yote kwa yote Makongoro hakutaka kuyatilia maanani,kwa sababu hakuwahi sikia popote kwamba bibi yake akituhumiwa kwa uchawi.
“Daah hapa sasa naanza kukihofia hiki kijiji…maana haya mambo niliyoyaona sio powa kabisa”
Alijisemea maneno hayo ndani ya nafsi kijana Makongoro,wakati huo akilivutia kichwani blanket yake aliyopewa na bibi yake kwa niaba ya kujifunika muda wa kulala…Na punde si punde alipitiwa na usingizi…
Hivyo basi baada Makongoro kupitiwa na usingizi mzito..Ghafla upepo mkali ulivuma nje ya nyumba ya Mzee baluguza,wakati huo Mzee baluguza yeye akiwa ameshaondoka zake katika majukum yake ya kichawi..Naam!Baada upepo ule mkali kuvuma kwa kasi zaidi,punde si punde alitua chini na ungo Mzee mwakipesile ambae alipewa jukum la kumuunganisha kijana Makongoro katika familia ya kichawi.
Hivyo Mzee mwakipesile,akiwa na mkoba wake pamoja na hirizi mbalimbal..huku kiononi akiwa amevaa vazi jeusi na kichwani akiwa amejifunga kitambaa chembamba chenye rangi nyekundu..hima alichukuwa kibuyu chake kidogo kilicho chakaa,halafu akanyoosha mkono wake juu ulieshika kibuyu..kisha akaushusha….Ambapo alichukua kitu kama mkia wa ng’ombe mfupi,akawa anapitisha juu ya kile kibuyu mfano wa mtu anae fukuza nzi ili wasitue kwenye kibuyu..Hivyo baada kufanya hayo alikipuliza kile kibuyu kwa kutumi kinywa chake..kisha akacheka kidogo huku akikitazama kile kibuyu.
Na mala baada kumaliza kucheka,hatimae Mzee mwakipesile aliinamisha kichwa chini kidogo…punde tu akawa amepotea pale nje,ghafla akawa ameibukia ndani chumbani kwa Makongoro.
Hakika Mzee mwakipesile alitabasam kidogo baada kumwona Makongoro akiwa amelala kitandani hana hili wala lile…Na hapo ndipo alipopiga hatuwa kumfuata kitandani,ila kabla hajafanya jambo lolote kwa makongoro…Alimruka kwanza mala tatu kisha akasogea kando kidogo na kitanda alichokuwa amelalia Makongoro..Kwisha kufanya hayo,Hatimae Mzee mwakipesile alimwita Makongoro kwa ishara ya mkono,ambapo Makongoro aliweza kunyanyuka mwenyewe kutoka kitandani.Akiwa hajitambui alimfuata Mzee mwakipesile ambae nae alizidi kurudi nyuma mpaka alipo fika kwenye kona ya chumba..Hivyo akawa amepotea ambavyo ndivyo hivyo ilivyokuwa kwa Makongoro nae alipotea kama alivyopotea Mzee mwakipesile.
Basi mala baada Mzee mwakipesile kutoweka na Makongoro…hatimae alimpeleka kwenye milima mikubwa ya kijiji cha bhonde..ambapo huko kulikuwa na jopo kubwa la misukule iliyofugwa..Hivyo kijana Mkongoro akawa amekabidhiwa kazi ya kuilisha ile misukule..ambayo chakula chao kikuu ilikuwa ni ndizi mbivu pamoja na pumba za mahindi iliyochemshwa..kweli Makongoro aliifanya ile kazi aliyopewa na Mzee mwakipesile,kazi ya kuilisha misukule.Kazi ambayo Makongoro aliifanya akiwa hajitambui…kwa hakika Makongoro,kijana ambae alikuwa na mwili mdogodogo alipata shida kuilisha ile misukule,kwani kuna baadhi ya misukule ambayo ilikuwa na njaa kali ambapo ilimsumbua sana Makongoro.
Naam!Baada Makongoro kuhitimisha ile kazi,hatimae ile misukule ilipotea mmoja baada ya mwingine..mpaka pale yote ilipokwisha..hivyo punde si punde kundi kubwa la wachawi wakiwa na Nyugo zao(ungo)mfano wa kumbikumbi walitua katika ile milima ambapo waliwakuta Mzee mwajipesile pamoja na Makongoro..
Hivyo salam za kichawi ziliendelea pale,wakati huo Bi mazoea ambae ndio bibi yake Makongoro alionekana kushtuka baada kumwona mjukuu wake maeneo yale ambayo ni mahususi kwa niaba ya wachawi na misukule kulia chakula..Basi haraka sana Bi mazoea alimtafuta Mzee mwakipesile,kwani alijuwa kuwa dhahili shahili Makongoro atakuwa kaletwa na Mwakipesile na sio mtu mwingine.Kweli hatimae Bi mazoea alifanikiwa kumapata japo kwa mbinde kwa sababu wachawi walikuwa wengi mno.
“Habali bhabha”..Bi mazoea,mzee aliekuwa na mapengo alimsalimia kwanza Mzee mwakipesile huku akionekana kuwa na hofu…
“Salama tu kwema?..”Alijubu mwakipesile.
“Hapana sio salama…Hivi wewe ndio umekuja na mjukuu wangu?..”
Alicheka kwanza Mzee mwakipesile baada Bi mazoea kumuuliza hilo swali..kisha akamjibu.
“Ndio mimi..ila usihofu hapo alipo haelewi chochote,zaidi anahisi yupo kwenye ndoto tu kitandani”
“Mmmh wewe acha utani bhana..embu mtazame kwanza…eti eti etiii…mbona ananichekea ..Aaaa..We mzee mwakipesile usinisababishie matatizo mimi..onhooo”
“Acha woga basi..yani ulivyo kama sio nguli wa uchawi?..usiniabishe Bi mazoea mpenzi wangu wa zamani sawaeee”
Aliingiza utani kidogo Mzee mwakipesile,lakini Bi mazoea hakucheka wala kutabasam kwani alighazibishwa na kile kitendo alichokifanya Mzee mwakipesile.
“Haya??..ila nadhani unamjuwa vizuyi babu yake..mimi sina neno”
Hakika kwa sauti ya upole Bi mazoea alimwambia hivyo Mzee mwakipesile…Naam! Mzee mwakipesile baada kuambiwa hivyo,haraka sana aliandaa ungo wake kwa niaba ya kumrudisha Makongoro nyumbani kwaa maana alikuwa akimwogopa sana Mzee baluguza,yote kutokana na uchawi mkali aliokuwa nao Mzee baluguza ambae ndio babu yake makongoro..Basi wakati Mzee mwakipesile alipokuwa akifanya harakati za kuondoka ,ghafla alizuiwa asiondoke mpaka ale chakula kwa pamoja,chakula ambacho kilikuwa na nyama za binadam kinywaji kikiwa ni dam za binadam..Hivyo basi Mzee mwakipesile alilia hatimae alipewa ruksa ya kuondoka,huku wakimuhiza awahi kwa sababu watakuwa wakimsubili yeye pekee,kitendo ambacho kilimlazim Mzee mwakipesile kuahilisha kutumia nyia ya ungo,akawa ametumia njia ya kupotea kama mwanga uzimikapo.
Kweli punde si punde Mzee mwakipesile alitua kwenye uwanja wa nyumba ya Bi mazoea mke wa Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro…Faster alifanya mambo kama aliyoyafanya hapo awali wakati wa kumchukuwa Makongoro…Na hatimae akawa amemrejesha makongoro kitandani,lakini kabla Mzee mwakipesile hajaondoka chumbani kwa makongoro..ili asahi kula chakula na wachawi wenzake..Mala ghafla Mzee baluguza nae alitua mlemle chumbani kwa Makongoro..wakati huo Mzee baluguza na Mzee mwakipesile ni Maadui kama ilivyo maji na moto.
“Mwakipesile,hivi unanitafutia nini wewe mzee?..eeh nilishakwambia sihitaji upuuzi wako kwa mjukuu wangu mbona hunielewi?..$asa nadhani dawa yako moja kwanza lazima nikushkishe adabu mpumbafu”
Alikuwa ni Mzee baluguza…alisikika akiongea maneno hayo baada kumkuta mwakipesile chumbani kwa mjukuu wake,wakati huo nao Mzee mwakipesile alikuwa akijiweka sawa kwa niaba ya kupambana,kwani alijipa matumaini kwamba huwenda akafanikiwa kumshinda Mzee mwenzake baluguza ambae nae alikuwa si haba kwa mambo ya kichawi.
Kweli punde si punde walipotea mle chumbani kwa Makongoro..wakatua nje ya nyumba ambako kulikuwa na uwanja umpana….Hivyo haraka sana kila mmoja alifanya maandalizi yake ya kuvaa hirizi kwa ustadi wa hali ya juu..Na hatimae pambano likaanza…Aliekuwa wa kwanza kumuanza mwenzake alikuwa ni Mzee baluguza ambapo kwa kutumia mikono yake aliikunja kisha akaikunjua mfano wa mtu anae skuma gari…ghafla ulitokea moto ambao moja kwa moja ulimfuata Mzee mwakipesile…hivyo kwa kuwa Mzee mwakipesile nae alikuwa vizuri kwa yale mambo..Aliinama moto ule aliourusha baluguza ukawa umepitiliza………Alicheka Mzee mwakipesile halafu nae akajibu mashambulizi mawili ya haraka haraka…ambapo Mzee baluguza alitaka kujitahidi kulikwepa,lakini fataki moja ilimbabatiza.Fataki ambalo Mzee mwakipesile alilirusha kwa kutumia mdomo ambao uliweza kutema moto mkali malambili ya ule alio urusha Mzee baluguza…Hivyo Mzee balu akawa ameanguka Chini kama mzigo wa kuni..kitendo ambacho kilimfanya augulie maumivu kwanza kabla hajajibu pigo,huku Mzee mwakipesile akiendelea kujiweka sawa wakati huo akimwita Baluguza ili amkomeshe vizuri.
“Khaa uchawi huu kautoa wapi huyu mzee!..hakika leo nimeumbuka…ila ngoja nijitahidi la sivyo huyu mzee atamzoea mjukuu wangu”
Ni mzee baluguza alikuwa akiyaongea hayo maneno,wakati bado akiwa chini akiendelea kuugulia maumivu…ila mwishowe alisimama kisha akarusha moto kwa kutumia mkono wake wa kulia ghafla Mzee mwakipesile akaunasisha pamoja na moto wake,haraka sana Mzee balu alirusha tena moto kwa kutumia wa kushoto…hivyo kwa kuwa nguvu zote za mzee mwakipesile zilikuwa zikitumika upande mmoja ambao ni kuugandisha moto pamoja na mokono wa kulia wa buluguza…Hatimae ule moto uliorushwa na mkono wa kushoto ulifkia Mzee mwakipeslile……Alilalama kwa sauti kali kali huku akigagaa chini..Sauti hiyo iliweza kumfikia mkuu wake wa kichawi kule milimani ambako ndiko kulikokuwa na makazi maalum ya kulisha chakula misukule pia na wachawi kulia chakula.Hivyo mkuu yule baada kuiskia hiyo sauti ya Mzee mwakipesile alishtuka..hima alimwita mchawi mmoja kisha akamwagiza amletee chungu,kweli punde si punde yule mchawi alikileta..ambapo mkuu yule ambae jina lake ni Bi kileleganya alifanya mambo yake ya kichawi…ghafla ndani ya kile chungu kilichokuwa na mkojo wa mama mjamzito,walionekana Mzee baluguza na mzee mwakipesile wakipigana.Wakati huo Mwamipesile akionekana kushambuliwa sana.
“nyote kimyaaaa” Bi kileleganya ambae ndio mkuu wa wachawi pale kijijini bhonde,aliutuliza umati wa wachawi ulikuwepo pale milimani…kweli wote walikaa kimya
“Mnaongea ongea tuuuu…mnajuwa kinachoendelea muda hu?..”
Aliongeza kwa kusema hivyo mkuu yule wa wachawi..ghafla wote walianza kutazamana.
“sijawaambia mtazamane…pumbafu zenu..haya haraka sana kila mmoja ajiandae,safari moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Bi mazoea tukamwokoe mwenzetu…”
Amri ilimtoka kwa mkuu wa wachawi huku akionekana kukasilika…hivyo punde si punde wachawi wote walikuwa wameshakaa kwenye nyungo zao tayali kwa safari ya kwenda kumwokoa Mzee mwakipesile ambae alikuwa akipigwa vibaya na Mzee baluguza.
Mfano wa mbayuwayu warukavyo angani ndivyo ilivyokuwa kwa wale wachawi jinsi walivyopaa angani na nyungo zao…naam!punde si punde wachawi wale wakawa wanefika,ila walitua pembeni kidogo kisha wakapanga mikakati jinsi ya kumwokoa mwenzao..Hivyo wote kwa pamoja walikubaliana kumvamia Mzee baluguza kasoro Bi mazoea ambae ni mke wa mzee baluguza..Hakika patishika nguo kuchanika, ugomvi uliendelea pale lakini mwishowe wale wachawi walimvamia wote kwa pamoja baluguza..na kwa kuwa baluguza alikuwa ameshachoka alishindwa kujitete kwa kutumia mikono yake,hivyo aliita nyuki wa kichawi ambao alikuwa amewafuga…kweli punde si punde sauti za nyuki ziliskika wakija kwa kasi,kitendo ambacho kiliwafanya wale wachawi kutimka lakini hawakumwacha Mzee mwakipesile ambae alikuwa kapigika vibaya.
Baada ya hayo kupita,Mzee baluguza alirudi ndani kulala akiwa hoi bi taabani..wakati huo kabla hapajakucha Makongoro nae aliamka ili aende chooni kujisaidia..Alistaajabu baada kujikuta mwili umechoka bila kufanya kazi yoyote ngum,lakini hakutaka kujaji sana zaidi alishuka kitandani kisha akaelekea chooni kujisaidia…hakuna asiejuwa vyoo vya kijijini jinsi vilivyo..makongoro wakati anatembea kuelekea chooni ghafla alimwona paka mkubwa mweusi mbele yake,,alimfkuza lakini hakutoka…..Hivyo Makongoro akaamua kuchukua jiwe kisha akampiga yule paka mbae nae alilia kwa sauti kali kama mtoto huku akimfuata mbio makongoro.
“Bibi nakufaaaa”…Sauti ya makelele iliskika kutoka kwa Makongoro huku akikimbilia ndani..waakati huo yule paka aliepigwa jiwe alikuwa akimfukuzia nyuma..Lakini kabla yule paka hajamkalibia,ghafla alipotea…Hivyo hata mzee baluguza alipotoka nje kuangalia kilichomkuta mjukuu wake,hakuona chochote…Na hapo ndipo alipo mtuliza kumwondoa hofu,wakati ho tayali haja ya kwenda chooni kujisaidia ilikuwa imeshapotea kwa Makongoro.
Asubuhi ilipo ingia kabla Mzee baluguza na familia yake hawajaamka,ghafla mlango wa nyumba yake uligongwa…hivyo Mzee balu baada kuiskia hodi aliamka ili akamsikilize huyo mtu aliedamkia kwake..Baada kufungua mlango,alikutana uso kwa uso na Mzee mmoja ambae aliitwa kinono Mzee ambae pembeni yake alikuwa na kijana wake mdogo mwenye umri kama miaka kumi na nne…kijana huyo alikuwa ameshika kichwa chake ambacho kilikuwa kikitilisha dam.
“Habali za hasubui mzee baluguza”
“Salama tu sijui kwako!?..”
“Kwangu sio salama kiukweli…Kama unavyomwona kijana wangu jinsi alivyojileruhiwa na mjukuu wako..”
“Mjukuu wangu??..embu acha utani basi kinono..mjukuu wangu hajawahi kugombana na mtu yoyote hapa kijijini,kwahiyo wewe unapo niletea hizo tarifa zako naona kama unanichefua”
“Nakuchefua?..jana wakati kijana wangu alipokuwa kwenye matembezi yake,alipigwa jiwe na mjukuu wako,halafu leo hii unaniambia nakuchefua?..aaah wapi Mzee baluguza siku zote mimi huwa mstarabu lakini ukiniudhi na mimi ntakuudhi mala mbili ya ulivyo niudhi…hivyo basi mimi naondoka lakini nakuomba umkanye mjukuu wako,awe makini hapa kijijini la sivyo utamkosa…”
“Aaah mkwala huo..wewe mzee kinono huwezi kunitisha mimi wala mjukuu wangu,na kwa taarifa yako endapo kama mjukuu wangu akikutwa na tatizo lolote..hakika ntadili na wewe mpaka mwisho..mpumbaffu wewe”
ITAENDELEA
Sehemu Ya Pili (2)
Ilikuwa ni vita ya maneno kati ya Mzee kinono na Mzee baluguza,chanzo akiwa ni Makongoro ambae jana yake usiku alimpiga paka jiwe pasipo kujuwa kwamba alimpga binadam.
Hivyo mala baada Mzee kinono kuondoka zake na kijana wake,Mzee baluguza alirudi ndani akiwa na mawazo chungu nzima..kwani tayali alijikuta akibeba mzogo mzito wa kumlinda mjukuu wake ambae alikuwa akiwendwa na wachawi wawili tofauti,mmoja ambae ni Mzee mwakipesile,yeye alikuwa akimuwinda Makongoro kwa niaba ya kumwingiza kwenye familia ya kichawi,wakati huo Mzee kinono yeye alikuwa akimuwinda kwa niaba ya kumwondoa kabisa duniani..yote hayo akiwa ameyataka Mzee balu baada kutoa kauli mbaya kwake.
Basi mapigo ya moyo yalimwenda mbio Mzee baluguza huku kijasho chembamba kikizidi kumtilika katika mwili wake…Akiwaza atafanya nini ili kumlinda mjukuu wake ambae anaandamwa na wachawi..Hivyo wakati akiendelea kutafakari,ghafla Bi mazoae aliamka ambapo alishtuka baada kumwona mume wake kakaa kitandani huku akiwa amejiinamia.
“Babu makongoro…kulikoni mbona asubuhi mapema umejiinamia?..”
Bi mazoea alimuuliza hivyo mume wake baada kumwona kajiinamia..Lakini Mzee baluguza hakujibu chochote..aliinama uvunguni,akatoka na jungu kubwa kukuu ambalo alitoka nalo mpaka nje..kisha akachukuwa vibuyu vyake vidogo pamoja na hirizi..wakati huo Bi mazoea nae alitoka ndani..alishangaa baada kumwona mume wake akihangaika na Uchawi asubuhi,badala ya kwenda shamba kulima.Hivyo maswali mengi alijiuliza kichwani mwake ambayo alishindwa kuyapatia majibu.
“Babu makongoro,ebu nenda shamba bwanaa hayo mengine utayafanya ukitoka shamba..”
Bi mazoea alimwambia hivyo mume wake kwa msisitizo.
“Aaaah Bi mazoea..staki uniharibie siku sawa kama namnagani vipi nenda mwenyewe kwani huwezi?..”
Kwa hasira kali..akiwa amemkazia macho Bi mzoea,mzee baluguza alijibu hivyo..Ambapo Ili mbidi Bi mzoea kukaa kimya huku akimtazama mumewe alichokuwa akikifanya..lakini mwishowe aliishia kuguna kisha akarudi ndani kumwamsha Makongoro ili anawe..anywe chai.
Punde si punde Makongoro aliamka,akilalama viungo vya mwili wake kuchoka bila kufanya kazi..ghafla alitaharuki baada kujikuta akinukia harufu pumba iliyo chemshwa..Alijiuliza wapi alipoitoa ile harafu lakini hakupata jibu..asijue kuwa asiku alipelekwa na Mzee mwakipesile kuilisha misukule chakula ambacho kilikuwa ni pumba za mahindi iliyochemshwa..
“Mmh hii harufu nimeitowa wapi sasa??…Ee mbona sielewi?.”
Alijiuliza Makongoro huku akijinusa mikono yake mala mbili mbili..Wakati huo Mzee baluguza akiwa amesha changanya dawa ya kutoonekana kwa macho ya kawaida,kwani alifanya vile ili afanye mambo yake kwa uhuru bila kuonwa na Mjukuu wake ambae ni Makongoro.
Hivyo kwisha kufanya kila kitu kilicho wezekana,hatimae Mzee baluguza alijirudisha katika hali yake ya kawida..ambapo aliweza kujumuika na Makongoro kunywa chai na magimbi.
“Shkamoo babu..”
“Malakhabaa umeamkaje mjukuu wangu”
“Daah salama tu babu..ila najiskia kucho….” kabla Makongoro hajamaliza sentensi yake,ghafla Bibi yake alidakia “Makongoro magimbi yakiisha njoo uongeza..”
“Sawa bibi” Alijibu makongoro haraka,huku akitaka kumwambia babu yake,vile anavyojiskia mwili.
“Eeh ulikuwa unataka kusema!?..”
“Nilitaka kusema kwamba najiskia kuchoka mwili mzima..harafu istoshe mikono yangu inatoa harufu ya pumba iliyo chemshwa..yaani hapo nilipo hata sielewi kwanini”
Makongoro alimwambia hivyo babu yake,lakini cha ajabu mzee baluguza alimtazama Bi mazoea jicho ngebe huku akiaahirisha kula magimbi..moja kwa moja alisogea mpaka mahali alipokuwa amekaa Bi mazoea akila magimbi.
“Nadhani umemskia mjukuu wako jinsi anavyo lalamika..sasa nakwambia wewe,ili ukawaambie Wenzako kwamba staki michezo yenu kwa mjukuu wangu…Chezeeni vijana wa hapa hapa kijijini sio huyu sawaaa”
Kwa sauti ya upole Bi mazoea aliitikia “Sawa”
Wakati huo Mzee baluguza akijiandaa kuelekea shamba..hivyo kufumba na kufumbua alipotea pale nyumbani kwake,akatokea shambani ambako aliendelea na Shughuli zake.
Naam!mchana shwari usiku shali katika kijiji kile bhonde..hatimae usiku uliingia ambapo ilipotimia saa nne usiku,iliskika mbiyu ya kichawi ..Mbiyu ambayo iliwafanya wachawi wote wa kijiji bhonde kufaham kuwa usiku wa manane kutakuwa na kikao.. kasoro mzee baluguza hatokuwemo kwa sababu alikuwa na uchawi wa kujitegemea.. Kweli saa saba usiku ilipotimia,wachawi wote walikusanyika chini ya ule mti mkubwa kuliko yote kijiji kizama..Na punde si punde Bi kileleganya ambae ndio mkuu wa wachawi alifungua kikao ambacho kilijadili mstkabali wa kumwangamiza Mzee baluguza ambae kwa namna moja ama nyingine alionekana kikwazo kwao..Hoja ambayo iliungwa mkono na wachawi wengi haswa walipokumbuka lile shambulizi la nyuki wa kufungwa..ila Bi mazoe ambae nae alikuwemo kwenye kikao hakuiafiki hiyo hoja,lakini alishindwa kuzungumza kwa sababu asilimia tisi na nane walilipendekeza hilo suala..
Na wakati hayo yakijili….Nyumbani kwa baluguza..Alitokea Mzee kinono baba wa kijana aliepigwa jiwe na Makongoro,mzee ambae alikuwa na uchawi wa kujitegemea kama ilivyokuwa kwa Mzee baluguza.
Hivyo basi mzee kinono alitua nje ya nyumba akiwa katika mavazi ya kichawi…na nakabla hajafanya jambo lolote alikunjua kiganja chake akatazama usalama wa eneo alilo simama..Alicheka baada kujikuta yuko salama,hivyo kazi ikawa imebaki moja tu ya kumwangamiza makongoro ambae alikuwa amebaki ndani peke yake..Wakati huo Mzee baluguza nae alikuwa amekwenda nyumbani kwa mzee kinono kumwangamiza kabla hajammaliza mjukuu wake..hivyo wakawa wamepishana angani..pasipo wao kujuwa.
“Lazima niondoke na kichwa chake”
Alisema Mzee kinono.
Baada Mzee kinono kusema kuwa anaondoka na kichwa na makongoro,mwishowe aliamua kumfanyia vituko kwanza kabla hajamfanya jambo baya…ambapo alichukua hirizi yake kisha akaanza kuisugua sugua huku akiongea maneno ya kirugha,punde si punde Makongoro alinyanyuka kutoka kitandani..akatoka nje.
Mzee kinono alitabasam baada kumwona Makongoro,haraka sana alimmwagia maji ya kichawi ambayo yalimfanya Makongoro kurudi katika hali ya kujitambua…wakati huo tayali amesha pelekwa kando kando ya mto maragagalasi,,ambapo huko alikutana na yule kijana wa Mzee kinono..kijana ambae alipigwa jiwe na Makongoro.
“Mwanangu huyu hapa mshenzi aliekupiga jiwe jana usiku,kwahiyo mfanyie jambo lolote unalo litaka..alafu mimi nimmalize kabisa”
Kijana yule wa mzee kinono alicheka baada baba yake kumwambia hivyo,hima alichukua bakora kisha akamcharaza..
Wakati Makongoro alipokuwa akipigwa fimbo,upande mwingine alionekana Mzee baluguza akihaha kumtafuta Mzee kinono ili amuue..lakini juhudi zake ziligonga mwamba,na hapo ndipo alipokumbuka kuwa Mzee kinono aliahidi kumfanyia kitu kibaya Mjukuu wake…kwahiyo baada Mzee balu kulikumbuka hilo suala,haraka sana alikaa kwenye ungo wake kisha akarudi nyumbani kwake ambapo moja kwa moja alipitiliza Chumbani kwa mjukuu wake…ghafla alishtuka baada kumkosa mjukuu,hivyo alijuwa dhahili shahili Mzee kinono atakuwa amekuja kumchukuwa…Naam!bila kupoteza muda,mzee balu aliingia uvunguni mwa kitanda chake,akatoka na jungu lake kukuu lilokuwa likitunza vikolokolo vya kichawi..kisha akatoa filimbi yake ambayo alitoka nayo nje ya nyumba..hivyo akaipuliza kwa sauti kali,sauti ambayo iliwaita nyuki wake pamoja na bundi..ambapo Mzee kinono alimtuma yule bundi akamtafute Makongoro alipo ili aje atoe taarifa.
Kweli baada yule bundi kuondoka,ndani ya nusu saa alirudi moja kwa moja alitua kwenye bega la Mzee balu..hivyo nae mzee balu alimchukua kisha akamtazama kwenye mboni..Alishtuka baada kumwona Mjukuu wake akichapwa bakora na kijana wa Mzee kinono.
Haraka sana Mzee baluguza alipanda kwenye ungo wake huku jopo la nyuki likimfuata nyuma..punde si punde alitua pale pale kando ya mto maragarasi,ambako ndiko alipokuwa Makongoro akichezea kichapo kutoka kwa kijana wa Mzee kinono alihali Mzee kinono nae akiwa pembeni aktazama.
Lakini wakati yule kijana alipokuwa akiendelea kumchapa Makongoro,ghafla alistisha baada kuskia kuumwa na nyuki…Alitazama juu huku akiskia sauti ya kundi la nyuki likija mahali walipokua na baba yake wakimwadhibu Makongoro..na hapo ndipo walipoamua kutimua mbio wakimwacha makongoro,wakati huo mzee kinono akiamini kuwa kitendo cha makongoro kushambuliwa na nyuki ni adhabu tosha,kumbe asijue kuwa wale nyuki ni wa babu yake Makongoro ambae ni Mzee baluguza.
Baada Mzee kinono na kijana wake kutimka,mzee balu alifanya mambo yake ya kichawi ambayo yalimfanya Makongoro kutojitambua.Kisha akarudi nae nyumbani kwak…wakati huo Bi mazoea nae alirejea kutoka kweny mkutano wa kichawi,ambao ulikuwa ukijadili jinsi ya kumwangammiza mzee baluguza ambae alionekana kuwa kikwazo kwao.
Asubuhi ilipopambazuka,wa pili kuamka alikuwa ni Makongoro ambapo alishangaa kujikuta mwili umevimba bila kusjia maumivu..Lakini yote kwa yote alisubili babu yake bibi yake aamke ili amuulize tatizo nini,wakati huo akitafuta kibiriti ili akoke moto kwa sababu asubuhi ile palikuwa na baridi kali.
Hivyo mala baada moto kukolea vizuri..ghafla Makongoro aliitwa na bibi yake chumbani.
“Umeamkajekipenzi changu”..Bibi yake makongoro alimsalimia Makongoro huku akijifunga vizuri kitenge chake kifuani.
Hivyo makongoro nae alishusha pumzi kidogo huku akijiuliza atumie nafasi ile kumwambia bibi yake mambo yanamkuta kila siku au la!..lakini mwisho makongoro aliamua kunyamanza kimya,zaidi alimjibu bibi tu salam bibi yake.
“Nimeamka salama bibi..daah ila leo kuna bonge la baridi”
“Mmh kumbe ilikua hujui kama bhonde kuna baridi?..sasa nadhani umelijua hilo..”
“Kabisa bibi mimi siku zote nilikuwa sijui..”
“Sawa lakini si umkoka moto??..”
“ndio “
“Haya nenda kaote”
Makongoro alitoka ndani akimwacha bibi yake kitandani…wakati huo kule nje alipita Mzee mwakipesile akiwa na swala aliemnasa kwnye mtego wake..Hivyo baada mzee mwakipesile kumwona Makongoro,alimuuliza “Rafiki babu yako yupo?
Makongoro akiachia tabasam pana alijibu”Hayupo”
“Anhaaa haya twende nyumbani kwangu sasa tukale nyama ya swala”
Alisema hivyo Mwakipesile huku akipiga hatua za kuondoka…ambapo Makongoro aliweza kumfuata.
Kwa hakika Mzee mwakipesile alifrahi sana baada kuona makongoro kakubali kwenda nyumbani kwake,hivyo alijuwa tayali anaenda kukamilisha kazi aliyopewa na mkuu wake wa kichawi ambae alimkabidhi kazi ya kumvuta Makongoro kwenye familia ya kichawi.
Upande mwingine taarifa za kumuua Mzee baluguza zilienea kila club cha pombe pale kijijini ..kwani waliamua kutumia njia hiyo kwa sababu waliona hawataweza kumuua mzee balu kwa nguvu za Kichawi…bali pombe pekee kwa maana Mzee baluguza alipenda sana pombe .
Kweli ilipotimia saa nane ya Mchana…Mzee baluguza alirudi kutoka shamba,hivyo kwa kuwa alikuwa na kiu ya pombe aliamua kupita kwenye banda la pombe kabla ya kufika nyumbani kwake…Ambapo baada mpimaji wa pombe kumwona mzee balu,,alikumbuka taarifa zilizo sambaa za kumuua huyo mzee..hivyo kabla ya kumpimia alizunguka nyuma ya banda akafungua fundo la uchawi aliokuwa nao kwenye khanga,kisha akarudi kwenye kitengo chake..wakati huo Mzee balu alikuwa nje akiweka oda ya nyama ya mbuzi ya kuchomwa ili achachue mdomo…Kitendo ambacho kilimfanya yule mama mpimaji wa pombe kuweza kutia uchawi kwenye pombe ya mzee balu bila wasiwasi wowote.
“Mmmh…aaaa….naaam leo nimekubali pombe yako iko vizuri….!!..karibu nyama au huli nyama ya mbuzi?..”
“Apana we kula tu mi nikila natokwa na vipele mwili mzima” Alijibu mama muuza pombe..ambapo mmzee baluguza aliachia cheko kubwa kisha akasema
“Tatizo lenu uchawi mwingi hiki kijiji…ona sasa wanakuroga hadi kula nyuma ya mbuzi??..Daah”
Aliongea hivyo Mzee baluguza wakati huo akiendelea kunywa pombe yake….Na baada kumaliza alilipa kisha akaondoka zake nyumbani huku mkono akiwa na nyama choma kidogo aliyobakisha,,akimpelekea mjukuu wake ambae nae alikuwa kwa Mzee mwakipesile akila nyama.
Lakini wakati mzee balu alipokuwa njiani akirudi nyumbani kwake ,ghafla alihisi tumbo kumuuma..ambapo alishindwa hata kutembea,na punde si punde alianguka chini huku mapovu yakimtoka mdomoni na mkono wake wa kushoto ukionekana kukamitia hirizi kwanguvu.
Basi baada kuikamatia hirizi yake vizuri mkononi..mwishowe Mzee baluguza aliiachia baada maumivu ya tumbo kuzidi…hivyo akawa ameshika tumbo lake kwa mikono yake,wakati huo nguvu polepole zikizidi kumwishia.
Hakika Mzee baluguza alipasa sauti ya kuhisi maumivu…ila mwisho aliamua kukaa kimya kisha akajikaza kiume,ambapo alinyoosha mkono wake kuifuata hirizi yake aliyokuwa ameiachia…Baada kuikamata kamata,hatimae aliitemea mate mala tatu huku akiongea kirugha…Ghafla alitokea bundi wake wa kichawi ambae alikuwa amemfuga..Ambapo mzee baluguza alimshika kisha akamtazama kwenye mboni…Cha ajabu ulitokea mwanga mkali kwenye macho ya Mzee baluguza.Mwanga ambao ulienda kugonga kwenye macho ya yule bundi..Hivyo punde si punde yule bundi akawa amepotea akimwacha Mzee baluguza akiendelea kuvuja jasho jembemba la maumivu ya sumu aliyowekewa kwenye pombe pasipo yeye kujuwa.
Kweli baada ya nusu saa yule bundi alitua mbele ya Mzee baluguza huku akiwa na mkoba mdogo.Mkoba ambao ndani yake ulikuwa na dawa za miti shamba pamoja na hirizi mbalimbali..Hivyo Mzee baluguza alitabasam kwa mbali baada kumwona bundi wake kafanya kama alivyomwelekeza,na hapo sasa kazi ikawa imebaki moja tu ambayo ni yeye mwenyewe kuyaokoa maisha yake…
Lakini kabla Mzee baluguza hajafanya jambo lolote la kuweza kuyaokoa maisha yake kwa kutumia dawa zake..ghafla alitokea Mzee kinono..Mzee ambae alikuwa akimuwinda Makongoro mjukuu wa mzee baluguza ili amuue..wakati huo Mzee baluguza nae alikuwa akimuwinda kinono ili amuue kabla hajamuua mjukuu wake..Hivyo kile kitendo cha Mzee kinono kumkuta Baluguza hoi bitaabani..ilikuwa ni neema kwake kwani aliachia cheko kubwa kisha akasema.
“Mzee baluguza wewe mkubwa kiumri ila kiuchawi wewe bado mtoto sana…tazama sasa unakufa hivi hivi unajiona”
Aliongea maneno hayo Mzee kinono ambae alionekana kuvamilia mavazi ya kichawi..huku akimzunguka Mzee baluguza alielala chini akiwa hajiwezi.
Basi baada Mzee kinono kusema maneno hayo alichuchumaa chini kisha akauchukuwa ule mkoba ulioletwa na Bundi wa Mzee baluguza…akatwa mikononi mwake kisha akaongeza kwa kusema.
“Baluguza usijifu unambio bila kumwangalia anae kukimbiza…hivyo labda niseme neno juu yako..sihitaji lingi kutoka kwako huna viwango vya kupambana na mimi ambae nina uwezo wa kusafiri kila sehem hapa duniani…sio wewe mwisho wako sumbawanga ukienda mbali Congo halafu unajiaifu…”
Aliongeza kwa kujingamba hivyo Mzee kinono juu ya baluguza ambae tayali alionekana kukubali kifo…Na baada kusema hayo hatimae Mzee kinono alikunjua kiganja chake,ambacho kilitoa taswila jinsi Makongoro alivyokuwa akila nyama na Mzee mwakipesile…Hivyo alimwonyesha Mzee baluguza,,kisha kinono akasema “nilipanga nimmalize mjukuu wako..ila nabadilisha maamuzi ngoja nianze na wewe kwanza kisha nidili na mjukuu wako..”
Alisema hivyo Mzee kinono..wakati huo Mzee bulu akihusi kupata nguvu baada kumwona Mjukuu wake yupo kwa mwakipesile ambae nae alikuwa ni Mchawi.
Basi upande wa pili nako kule klabuni..yule mama aliemfanyia unyama Mzee baluguza kwa kumuwekea uchawi kwenye pombe ili amuue..hatimae aliweza kuwatangazia baadhi ya walevi waliokuwepo pale klabuni..
“Jamani nitoboe ni sitoboe..?
Alisema hivyo kwa furaha yule mama muuza pombe ambae alifahamika kwa jina la Mama chiku.
“Duuuh naona leo umeuza sana mpaka unaonekana kuwa na furaha kiasi hicho??? ..” Mmoja ya walevi alidakika kwa kusema hivyo..Lakini Mama chiku aliendelea …
“Mimi nauliza nitoboe nisitoboe..”
“Mmh huwenda leo kuna pombe ya bure hapa maana wewe mwenyewe si unamwona jinsi alivyokuwa na furaha..”
“Eeh kweli…ngoja tumwitikie..”
Zilikuwa ni sauti za walevi zilizokuwa zikiskika kwa kunon’gona…Na hatimae mmoja kati ya wale waliokuwa wakinong’ona alinyanyuka kisha akapasa sauti akisema..
“Jamani tusiwe na viburi…Hatuwezi juwa huwenda mama chiku leo anatoa zawadi ya pombe kwa hiyo tumwitikie jamaniii”
Hakika kicheko kikubwa na vikohozi vya kubanja…Vilisikika kutoka kwa walevi waliokuwepo pale klabuni…Na hapo ndipo sauti ya pamoja ilipo fuata ikisema “Toboaaaaaaa”
“Aaanhaaa habari njema ni kwa..aambaa yule Mzee anaejifanya anaujuwa sana Uchawi kuliko wengine,leo nimemnasa..”
Baada kusema hivyo yule mama muuza pombe..Ghafla walevi wote walipigwa na butwaa huku wakihoji “Nani huyo?..”Embu tuambie basi”
“Si huyu Mzee mwenye kijukuu kilichoka mjini”
Alijibu hivyo Mama muuza pombe.
“Anhaa kumbe huyu Mzee baluguza!..”
“Eenhee huyo huyo…kwa uchawi huu wa jumlajumla niliomuwekea,sijui kama kwake kafika”
Hakika yule mama chiku alionge kwa kujiamini…kwa maana alitimiza agizo la mkuu wa wachawi..agizo alilotoa la kumwondoa Mzee baluguza duniani kwa sababu alikuwa ni kikwazo kwao.
Hivyo upande mwingine nao alionekana Mzee mwakipesile akiwa na Makongoro,huku wakila nyama choma ya swala..wakati huo story mbali mbali zikiendelea.
“Mmh nyama hii tam sio Mchezo..”
Aliongea Makongoro huku akiwa ameshikilia nyama kubwa isoyokuwa na mfupa.
“Ee ukiskia swala ndio huyu bwana…hivi huko mjini kuna swala kweli??..” Mzee mwakipesile nae aliongeza kwa kusema hivyo..Kitendo ambacho kilimfanya Makongoro kucheka kwanza kabla ya kumjibu Mwakipesile.
“Daaah.. babu unachekesha sana..we umeshasema Mjini,sasa mjini mapori ya kuishi swala yanatoka wapi??..”
“Duh kwahiyo huko mjini hakuna hata pori la kuwinda sungura au kanga”
“Babuuu kule hakuna vitu kama hivyo…yani kule unapishana na magari tu..”
“Kha yani sehem kama hiyo me siwezi kuishi..kwa sababu sitoweza kuka siku mbili bila ku…”..Kabla Mzee mwakipesile hajamalizia Sentensi yake,ghafla Makongoro alidakia kwa kusema. “Babu geuza kwanza hiyo nyama inaungua”
“Aah kiukweli rafiki uko vizuri” Alijibu Mzee mwakipesile..na hivyo wote wakawa wamecheka.
“Enhe malizia sentensi yako sasa maana nilikukatisha..Sijui ulitaka kuongea nini”
“Anhaa sawa subiri niende chooni kwanza kujisaidia”
Mzee mwakipesile alimjibu hivyo Makongoro,kisha akaelekea nyuma ya nyumba yake ambako huko alinyoosha Mkono wake juu huku akiongea maneno ya kirugha..Ghafla kwenye ule mkono wake aliounyoosha ilitokea hirizi kubwa kiasi ambayo nayo aliifumua..kisha ukatoka unga mweusi ambao ndio uchawi.
Hivyo baada kuuchukuwa ule uchawi..Uchawi ambao ulikuwa mahususi kwa niaba ya kumvuta mtu kwenye familia ya kichawi..Hatimae Mzee mwakipesile alirudi ndani kwa niaba ya kumaliza agizo alilopewa na mkuu wa kichawi.
Hivyo aliingia ndani..akapitiliza mpaka jikoni ambako alimwacha Makongoro akila nyama,lakini cha ajabu Mzee mwakipesile hakumkuta..Ila hakukata tamaa,haraka sana alitoka ndani kisha akazipiga hatua kufuata njia ambayo ilikuwa ikifika nyumbani kwa Mzee baluguza..ambako ndiko Makongoro alikokuwa akiishi.lakini yote kwa yote hakufanikiwa kumwona..kiukweli Mzee mwakipesile alilaani kile kitendo cha Makongoro kumtoroka,kwani aliamini kua tayali anakwenda kuhitimisha kile kitu ambacho mkuu wake wa kichawi alicho mtuma.
Upande mwingine nako,katika mapori alionekana Makongoro akatimua mbio…Mbio ambazo alikimbia bila kugeuka nyuma..Kumbe wakati mzee mwakipesile alipo muaka Makongoro kwamba anakwenda chooni kujisaidia…Huku ndani alikobaki Makongoro akiendelea kula nyama ya swala,ghafla ulipita msukule kando yake..Kitendo ambacho kilimfanya Makongoro kutimua mbio kwa kupita njia za porini kuhofia kufatwa na ule Msukule.
Hivyo mala baada kufika nyumbani,alimkuta bibi yake akimenya viazi kwa niaba ya Chakula cha usiku…Bi mazoea alishtuka baada kumwona mjukuu wake kaja hima..na hivyo akawa amemuuliza kinacho msibu,lakini cha ajabu Makongoro alitabasam..tabasam la woga kisha akasema..”Mmh hamna bibi nilikuwa nafanya mazoezi tu..siunajuwa sisi watoto tulio zaliwa na kukulia mjini??…yaani tunapenda mwili mda wote uwe umechangamka…”
Alisema hivyo Makongoro,huku akitingisha mabega yake mfano wa mtu anajiweka sawa kwa niaba ya kupigana…Lakini licha ya Makongoro kumjibu namna hiyo bibi yake,ila Bi mazoea bado alionyesha waswadi usoni mwake..Na hapo ndipo alipomuuliza mjukuu wake..”Kwani tangu Asubuhi ulikuwa wapi..maana kutwa nzima hujashinda nyumbani”
Makongoro aliinamisha uso wake chini huku akijifikilia jibu la kumdanganya Bibi yake…Na baada kulipa aliinua uso wake kisha akajibu”Nilishinda kulee kuangalia mpira..”
“Mmmh mpira??..Mpira gani ambao unachezwa kuanzia asubuhi mpaka jioni hii??…Makongoro mjukuu wangu bwana kua makini na hiki kijiji..Shauli yako”
Bi mazoea alimjibu hivyo mjukuu wake,akionekana kutolidhishwa na majibu ya Makongoro..na ndio maana akawa amempa tahadhari kuhusu kile kijiji…Tahadhari ambayo ilimjengea sintofaham kijana Makongoro..na hivyo akawa anajiuliza”Kwani hiki kijiji kikoje??…eeh na yule mtu wa kutisha nilie mwona ndani ya nyumba ya Mzee mwakipesile ni nani??..je,kwanini Babu aliamua kunikataza kuzoeana na yule Mzee mwakipesile,,Mzee ambae anaonekana ni mwema kwangu??…Dah ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya filauni..Ila najuwa ipo siku ukweli utafahamika”
Alimaliza kwa kujipa imani Makongoro,huku akiingia ndani kuchochea kuni jikoni..wakati huo kwenye mafiga kuna junguu kuu lililo sheheni viazi vitam.
Naam!.Hatimae usiku uliingia…hadi saa tatu inatimia Mzee baluguza alikuwa bado hajarejea nyumbani kwake…Kitendo ambacho kiliweza kumshtua Makongoro kwani alikuwa hajazoea ile hali ya babu yake kuchelewa kurudi nyumbani..Na hivyo makongoro akawa amemuuliza bibi yake mahali alipo babu yake..Lakini cha ajabu Bi mazoea alimjibu shortcut kwa kusema..”Kwani nipo nae..??..”
Alijibu hivyo Bi mazoea,akimjibu mjukuu wake …Ambapo Makongoro aliweza kushangazwa na lile jibu alilopewa na Bibi yake..Na ghafla alisusa kula akidai kwamba hatoweza kula bila kumwona babu yake.
Wakati huo Makongoro alipokuwa akisema hayo,tayali alikuwa amenyanyuka pole pole alianza kuzipiga hatua kutoka ndani huku akisema..”Lazima nikamtafute babu yangu haiwezekani hadi muda huu awe hajarudi nyumbani…”
Alisema hivyo Makongoro kwa sauti ya kuashilia kulia..Na punde si punde aliondoka zake..akimwacha bibi yake akimwita,lakini Makongoro hakuitika bali alizidi kuondoka.
Basi Makongoro alizipiga hatua zake,kuelekea klabuni akidhani kuwa huwenda babu yake alizidiwa na pombe..Akashindwa kurudi nyumbani…ila kabla hajafika pale klabuni,aliaskia sauti za za walevi na Nyimbo mbali mbali wakiimbi,,wakati huo sauti ya Mzee baluguza ikisika juu zaidi kuliko wengine..Na hivyo Makongoro alizidi kukazana kuelekea kule klabuni ambako ndiko kulikokuwa zikitokea zile sauti za walevi ambazo ndani yake ilisikika na sauti ya Babu yake ambae ni mzee baluguza.
Ila mala baada Makongoro kusogea kabisa jirani na kile klabu,ghafla zile sauti alizokuwa akiziskia zilipotea..Na punde si punde walitokea kundi la fisi…Fisi ambao walipiga hatua kumfuata Makongoro..Hivyo Makongoro nae baada kuona anafuatwa na kundi la Fisi,haraka sana alivua ndala kisha akatimua mbio kurudi nyumbani..wakati huo akipasa sauti ya kuomba msaada..
Basi wakati Makongoro alipokuwa akikimbia,mala ghafla alisimamishwa na mtu njiani..na hivyo makongoro akawa amesimama akijuwa kuwa huwenda yule mtu akamsaidia ..kumbe mtu aliemsimamisha hakuwa mwingine ni Mzee mwakipesile.
Na upende mwingine…Mbiyu ya kichawi ilila kijiji cha bhonde..kuashilia kuwa kuna kikao cha dhalula..na hivyo iliwalazim wachawi wote wiliokuwa na ratiba zao za kufanya mambo yao yakichawi ,kuzivunja na moja kwa moja walihudhulia kikao kile cha dhalula…Ambapo mala baada wachawi wote kukasanyika kwenye kile kikao..Walistaajabu baada kumwona Mkuu wao kuonekana kuwa na wasiwasi..hivyo walitulia kusubili kipi atakacho ongea..
Kweli mwishowe yule mkuu wa wachawi Bi kileleganya alishusha pumzi kwanza akasema ..”Jamani samahani sana tena sana kwa kuharibu ratiba zenu…ila licha ya kuharibu nadhani hii itakuwa faida kwenu..”mkuu yule alikohoa kwanza,wakati huo wachawi waliokusanyika kwenye kikao wakionekana kuwa na shahuku ya kutaka kujuwa kipi kilichotokea…Hivyo mala baada mkuu kumaliza kukohoa hatimae alihitimisha kwa kusema..”leo nilipata taarifa kwamba Baluguza kafa..jamani ondoeni hiyo imani..Mzee baluguza kaonekana leo jioni Sokoni akinunua uchawi kwa yule Mzee wa kimanyema kutoka Congo..Na tayali katangaza ubaya kwa mtu alietaka kumuua..Kwahiyo habari ipo hivo,nafunga kikao maana nina safari ya kwenda Gambosh usiku huu”
Alimaliza kwa kusema hivyo yule mkuu wa wachawi,kisha akapotea.
Basi hofu kubwa..nyuso za huzuni na wasiwasi zilitanda kwa wale wachawi waliohudhulia kikao kile cha zalula..wakati huo Mkuu wa kichawi alikuwa akijiandaa kupotea maeneo yale ili akajiunge na wachawi wenzake ambao waliahidiana kukutana sumbawanga kwa niaba ya kuelekea gambosh nchini Nigeria….Lakini kabla mkuu yule wa kichawi ambae ni Bi kileleganya hajapotea anga zile za kikao,ghafla alisikika Mama chiku akimwita mkuu wake,,ikumbukwe kuwa mama chiku ndio alietaka kumuua Mzee baluguza baada kumuwekea sumu kwenye pombe.
“Mkuuu samahani kidogo” Alisema hivyo Mama chiku huku akionekana kujawa na wasiwasi…wakati huo akizipiga hatua mbele kumfuata mkuu wake ili amwambie jambo alilokuwa nalo.
“Jamani kwani kunatatizooo?…au kunajambo lingine mtaka kulisema??..”
“Hapana mkuu hakuna tatizo,ila nina jambo dogo tu naomba unasikilize” Alijibu Mama chiku.
“Anhaa sawa sungumza nikaskia..”
Bi kileleganya Mkuu wa kichawi alimpa nafasi ya kuzunguza Mama chiku..ambapo nae baada kupewa nafasi,alianza kwa kusema..”Samahani mkuu..nadhani unafaham kuwa mimi ndio muhusika wa kutaka kumuua Mzee baluguza..kwahiyo nilikuwa naomba uweze kun..” Mama chiku aliongea hivyo huku akitetemeka..Na kabla hajamalizia sentensi yake,mala ghafla hirizi ya Bi kileleganya aliyokuwa ameivaa mkononi kama saa ilionekana kuhema kuashilia kuwa anangojewa yeye pekee katika safari ya kuelekea gambosh..kitendo ambacho kilimfanya apotee akimwacha Mama chiku akiangua kilio kwani alikuwa hajamaliza kile alichotaka kuongea.
Upande mwingine nako,alionekana Makongoro akihaha kuitafutanjia ya kurudi nyumbani kwao…huku nyuma yake wakionekana fisi wengi wakimfuata..Wakati huo Mzee mwakipesile ambae alimtokea Mwanzo alikuwa tayali kapotea..alielekea kwenye kikao ambacho kilikuwa kimeitishwa na mkuu wake.
Hvyo basi wakati kijana Makongoro alipokuwa akiendelea kuhangaika bila mafanikio ya kufika nyumbani…Ghafla aliaoneka Mzee baluguza akiwa na ungo wake,,ambapo moja kwa moja alitua nyuma ya mjukuu wake ambae alikuwa kachoka baada kukimbia mbio ndefu..Na mala baada kutua aliunyoshea kidole ungo..punde si punde ukawa umepotea..kwisha kuupoteza ungo wake,,,Mzee balu alizipiga hatua zake kumfuata mjuu wake.. Hatua ambazo alikuwa akipiga moja nyingine anapotea,anaibukia mbele…hivyo hivyo mpaka akamkalibia mjukuu wake..Ambapo aliunyoosha mkono wake wa kulia juu na punde si punde kwenye ule mkono alio unyoosha kilitokea kibuyu kidogo ambacho kilikuwa na nembo za ajabu..Alicheka Mzee balu baada kukiona kile kibuyu,,wakati huo akiushusha chini ule mkono ambao ulikuwa umeshikilia kibuyu….
Na baada kuhitimisha cheko lake,hatimae Mzee baluguza alimimina unga frani kwenye kiganja uliotoka ndani ya kile kibuyu kisha akaupuliza ule unga ambapo moja kwa moja ulimkuta Makongoro..Na hivyo ghafla akawa hajielewi,,kitendo ambacho kilimfanya Mzee baluguza kumbeba na kisha kuondoka nae huku akiusifu uchawi ule alioutumia kwa makongoro kwani hakuta kujionyesha kwa mjukuu wake yeye ni Mchawi.
Basi baada Mzee baluguza kutoweka na mjukuu wake…upande mwingine wale fisi waliokuwa wakimfukuzia Makongoro ghafla waligeuka kuwa watoto ambapo waliangua kicheko kikubwa huku wakigongeana mikono na kisha kucheza michezo mbali mbali ya kitoto…kumbe hakuwa fisi bali ni watoto ambao wazazi wao wanajihusishs na masuala ya kichawi.
Kwingine nako,,mzee baluguza alitua salama huku akiwa sambamba na Mjukuu wake ambae tayali alikuwa hajui kinachoendelea…na kabla hajamwingiza ndani,alirudia kuunyoosha mkono wake tena juu..ghafla uliotea mkoba chakavu ambao ndani yake kulikuwa na hirizi pamoja na zana mbalimbali za kichawi…Alirudia kutabasam Mzee baluguza huku akijisemea “Walinibpu sasa mimi nawapigia…sina utani..Ngoja nikamlaze mjukuu wangu kisha nianze msako..”
Alisema maneno hayo kijasili kabisa Mzee buguza huku akimkumbatia mjukuu wake,,na punde si punde alitokea chumbani kwa Makongoro…hivyo akawa amemlaza kitandani kwake kisha akamluka mala tatu ili kumzindua..
Baada kufanya hivyo Mzee baluguza aliingia chumbani kwake..moja kwa moja akazama uvunguni mwa kitanda alichokua akilalia,,Akatoka na jungu lake kukuu ambalo lilikuwa mahususi kwa kutunza mazagazaga ya kichawi…Wakati huo huo ulivuma upepo mkali kisha kwenye kona ya chumba alitokea Bi mazoea mke wa Mzee baluguza,,,ambapo mala baada kumwona mume wake yupo bize alishtuka kwani alijua tayali anaenda kulipa kisasi kwa mtu aliemuwekea Sum kwenye pombe kwa nia ya kutaka kumuua.
“Za saa hizi Babu Makongoro…” Bi mzoea aliamsalimia mume wake,lakini Mzee balu alinyamanza kimya bila kuijibu salam aliyopewa na Mke wake..kitendo ambacho kilifanya kimya kidogo kutawala ndani ya robo saa…Na mala baada Mzee balu kukamilisha kile alichokuwa akikifanya,aliinua uso wake kumtazam mke wake ambae nae alikua kitandani kalala..kisha Mzee balu akasema..” naondoka na ntakacho rudi nacho naomba ukawatangazie wachawi wenzako…pumbaffu mwanamke gani mwenye roho mbaya kama simba yani upo tayar mumeo nife ili mfrahishe nafsi zenu.. nakuchukia sana Bi mazoea laiti kama ungelikuwa binti mdogo basi ungerudi kwenu..”
Mzee baluguza alisema maneno hayo kwa hisia kali huku akijichora chora usoni kwake kwa niaba kwenda kulipa kisasi…Wakati huo Bi mzoea nae akiwa kimya kitandani akijifanya kasinzia huku moyoni akijisemea “Mahali yenyewe hadi leo hujanitolea kazi kuropoka…kufaa tu”
Aliongea ndani ya nafsi yake Bi mazoea..maneno ambayo laiti kama Mzee baluguza angeyaskia basi kinuka.
Basi Mzee baluguza alipotea mle ndani mwake…akajikuta yuko nje.Ambapo moja kwa moja alifanya ishara ya kuita ungo ambao ndio chombo kikuu cha kusafiria wachawi..punde si punde ungo ulitokea hivyo haraka sana Mzee balu aliweka katika ule ungo kila dhana ya kichawi…Akiwa katika vazi la kitambaa cheusi ambacho nacho alikivaa kiunoni,,hatimae mzee balu alipaa angani akiwa na ungo wake kuelekea kwa Mama chiku..mama muuza pombe ambae alitaka kumuua Baluguza kwa kumuwekea sumu kwenye pombe.
Lakini wakati Mzee baluguza alipokuwa angani akielekea kwa Mama chiku,,mala ghafla alidondoshewa bundi kwenye ungo wake,bundi ambae nae alirusharusha mbawa zake mda mfupi tu akawa amefariki…Mzee balu alishtuka baada kumwona yule bundi..alipomtazama vizuri aligundua kuwa ni yule bundi wake ambae alikuwa akimtuma kunasa taarifa mbalimbali..Hivyo roho ilimuuma sana Mzee balu kwa kumpoteza mtoa taarifa wake,wakati huo nyuma yake alionekana Mchaw mmoja akiwa na tochi mbili akimfuata kwa kasi baluguza.
Safari ya Mzee baluguza angani ilianza kuwa ya mashaka,baada kufiwa na bundi wake ambae alikuwa akimsaidia kunasa taarifa mbalimbali..wakati huo nyuma yake ikionekana touch mbili zikimfuata nyuma.
Hivyo baada Mzee baluguza kugundua kuwa anafuatwa nyuma,,haraka sana alifungua mkoba wake mdogo aliokuwa nao..kisha ndani ya ule mkoba alichukua hirizi yake kubwa kisasi,,ambayo nayo alijifunga mkononi huku akiongea maneno ya kirugha kitendo ambacho kilimfanya Mzee baluguza kugeuka popo…ambapo aliweza kuzikimbia zile touch mbili zilizokuwa zikimfuata nyuma.
Hatimae Mzee baluguza alifika nyumbani kwa mama chiku..mama ambae alithubutu kutaka kumuua…na hivyo ujio wake Mzee baluguza ni kutaka kulipa kisasi na sio kitu kingine.
“Lazima nifyeke kichwa chake mwanamke huyu mshenzi” Alisema Mzee baluguza huku akijiandaa jinsi ya kuingia ndani ya nyumba ya mama chiku.
Na mala baada kuwa tayali Mzee baluguza alipiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya mama chiku..ambapo baada kuifikia aliegemea ukata,haraka akajikuta yupo chumbani kwa mama chiku…akaweza kumwona mbaya wake akiwa amelala usingizi mzigo…na hiyo ndio ikawa nafasi ya Mzee baluguza kumfanyia unyama wa kutisha mama chiku kwa kumkata shingo yake huku dam akiikinga kwenye kibuyu chake ambacho nacho kilijaa…hivyo dam ya mama chiku ikawa bado inaendelea kusambaa akitandani… wakati huo mwili wake ukiendelea kurusha baadhi ya viungo vya mwili.
Baada kufanya kitendo hicho Mzee baluguza alicheka kidogo..kisha akanywa kidogo ile dam aliyokinga kutoka kwenye mwili wa mama chiku…ambapo baada kuimeza alitikisa kichwa kuashilia kuikubali kuwa dam ile ya mama chiku nitamu sana.
“mhm unadam tam sana wewe mwanamke..lakini tatizo lako moja tu,ulitaka kushindana na mwamba usiwezekanika…na ili nionekane kuwa mimi ni Shujaa!!ngoja niondoke na kichwa chako” Yalikuwa ni maneno ya kijasili ambayo Mzee baluguza alikuwa akiyaongea,,wakati huo akitumia kisu chake kuikata shingo ya mama chiku ilikutenganisha kichwa na kiwiliwili…hivyo ndani ya muda wa dakika mbili tayali Mzee baluguza alikuwa amefanikisha zoezi hilo…ambapo moja kwa moja alipotea mle chumbani kwa mama chiku..ghafla akaonekana nje huku mkononi mwake akiwa na kichwa cha mama chiku…ambapo alizipiga hatua mbili na kisha kupotea maeneo Yale ya nyumbani kwa mama chiku.
ITAENDELEA
Sehemu Ya Tatu (3)
Baada Mzee baluguza kupotea maeneo Yale..muda huo huo alitua Mzee kinono akiwa sambamba na ungo wake..Mzee kinono alionekana kumfukuzia Mzee baluguza lakini kwa bahati mbaya hakumkuta..”Daah huyu Mzee baluguza anauchawi wa nchi gani!? ila ipo siku tutakutana tu”
Alisema Mzee kinono…Mzee ambae alikuwa na bifu kali na baluguza…hivyo kwisha kusema hatimae,nae alipotea.
Asubuhi ilipopambazuka ngoma ya kuashilia msiba iliskika kijijini bhonde…Masikio ya wanakijiji yalitega vizuri ili waweze kuskia jina la mtu aliefariki kutoka kwa mtoa tangazo…nae mtoa tangazo la msiba hakuweza kusita kumtaja…nae hakuwa mwingine ni mama chiku.
Hakika wanakijiji walio isikia hiyo taarifa walionekana kustaajabu lakini kwa wale ambao walikuwa wachawi hawakuweza kushangazwa na kifo cha mama chiku kwani walijua sababu iliyomsababishia umauti.
Wanakijiji walijazana nyumbani kwa mama chiku kwa niaba ya mazishi..lakini kabla mwili wa mama chiku haujapelekwa kuzikwa,,mala ghafla alitokea Bi kileleganya ambae ni kiongozi…Na kitu ambacho alikifanya Bi kileleganya ni kuuzuia ile mwili wa mama. chiku usizikwe badala yake ukawe kitoweo kwa familia ya kichawi pamoja na misukule.
Hivyo Bi kileleganya kwa nguvu kubwa ya kichawi aliunyakua ule mwili wa mama chiku,,kisha akaweka mti wa mgomba..mti ambao kama huna macho ya kichawi huwezi kuugundua.
Mazashi yalifanyika..wanakijiji baadhi wakijua wamemzika mama chiku na wengine ambao walikuwa wachawi walijua dhahili shahili wamefukia mgomba wa ndizi.
Hivyo baada ya mazishi kumalizika…walionekana vijana watano wakikaa kikao cha muda mfupi..kikao hicho ambacho walijadili kufanya upelelezi ili kumpata mtu aliehusika na mauaji ya mama chiku…Hakika vijana wale ambao nao kiuchawi walikuwa si haba walikubaliana kulifanyia kazi hilo suala..na kisha wakashikana mikono wote kwa pamoja,wakawa wamepotea mfano wa taa izimikapo gizani.
Wakati vijana wale watano wakipanga kufanya upelelezi wa mauaji ya mama chiku…upande mwingine,,Wazee wateule wakishirikiana na serikali yakijiji walikaa pamoja kujadili mauaji ya kikatili yaliyofanyika kijijini kwao..ambapo walikubaliana kumuunguza ndani ya nyumba mtu atakae bainika kuhusuka na mauaji ya mama chiku.
Taarifa hiyo iliweza kumfikia chinichini Mzee baluguza ambae ndio muhusika…cha ajabu baluguza alicheka kwa dharau kisha akasema..”hii tayali imeshakuwa VITA ..sikutaka kumfundisha uchawi mjukuu wangu Makongoro lakini imebidi la sivyo Nitamkosa…ngoja leo usiku nimpeleke gambosh…hakuna namna”
Alijisemea maneno hayo Mzee baluguza huku akiungojea usiku kwa ham ili ampeleke mjukuu wake gambosh nchin Nigeria ili nae aweze kujilinda katika kijiji kile kilicho sheheni wachawi.
Hatimae usiku uliingia…ambapo siku hiyo familia ya Mzee baluguza…yaani Bi Mazoea ambae ni mke wa Mzee baluguza na mjukuu wao ambae ni Makongoro walilala mapema kwa sababu kijiji kilionekana kuchafuka baada kifo kile cha mama chiku ambae alikatwa shingo na Mzee Baluguza.
Hivyo saa Sita usiku ilipotimia..Mzee Baluguza alinyanyuka kutoka kitandani kwake,kisha akaingia uvunguni ambako alitoka na chungu chake alichokuwa akihifadhia mazagazaga ya kichawi…alikikamata kile chungu kwa mikono yake miwili..kisha akizipiga hatua kuelekea chumbani kwa mjukuu wake ambae ni Makongoro ,,wakati huo Makongoro alikuwa amelala fofofo.
Mzee Baluguza baada kuingia chumbani kwa Makongoro…alimwamsha nae Makongoro aliamka.
Baada Makongoro kuamka..Mzee Baluguza akimtazama mjukuu wake usoni kisha akasema “Nakuomba ufumbe macho yako..usifumbue mpaka nikuruhusu” Alisema Mzee Baluguza ,,wakati huo akimfunga hirizi mjukuu wake. Mara baada kumalizika zoezi lile,hatimaye Mzee Baluguza alimwambia Makongoro asimame.Makongoro alisimama huku akijiuliza babu yake anamaana gani kumkatisha usingizi na kisha kumfanyia Mambo Yale.
“nakuomba usifumbue macho…ukifumbua kabla sijakuruhu shauli yako…” Alisisitiza Mzee Baluguza akimwambia mjukuu wake.
Hivyo baada kumaliza hayo,,Mzee Baluguza alimwambia Makongoro amkumbatie..Makongoro alimkumbatia,ambapo punde si punde alijikuta wapo nje ya nyumba.
Mzee Baluguza alinyoosha mkono wake wa kulia,,ghafla kikatokea kibuyu chake kidogo ambacho ndani yake kilikuwa na damu, alikunywa damu ile iliyo kuwomo ndani ya kile kibuyu…Kisha akarudia kumwambia Makongoro “usifumbue macho macho,pia nikumbatie vizuri usiniachie” Makongoro alifanya hivyo.
Kwisha kusema hayo,walipaa angani…safari ya kuelekea gambosh ikawa imeanza.
Wakati walipokuwa angani…Makongoro alihisi baridi Kali pamoja na upepo mkali,,kitu ambacho kilimfanya kutaka kufumbua macho ili angalie yupo katika mazingira gani…lakini kabla Makongoro hajaifkia macho yake…ghafla alijikuta wametua aridhini…na hivyo Mzee baluguza alimruhusu Makongoro kuyafumbua macho yake.
Makongoro alishtuka baada kufumbua macho yake..kwani aliwashudia wachawi wapatao therathini ambao mavazi yao yalifanana na mavazi aliyoyavaa babu yake.
“Babu kwani hapa wapi” Alihoji Makongoro akimuuliza babu yake…Lakini cha kushangaza Mzee baluguza hakumjibu chochote mjukuu wake. Wakati huo ilisikika sauti kutoka ndani ya wachawi wale therathini ikisema “Jamani tuondokeni tayali tumetimia”
Ilisikika ikisema hivyo ile sauti,,ambapo iliweza kuungwa mkono na wachawi wote waliokuwa wamekusanyika pale rukwa kwa niaba ya safari y kuelekea gambosh.
Hivyo baada wazo hilo kuungwa mkono na jopo lile la wachawi…punde si punde alitokea mtokea Mzee mmoja ambae aliitwa mahulubila…ambapo baada kutokea Mzee yule..haraka sana alichukua kisu kidogo ambacho muda wote alikuwa nacho mfukoni…kisha akatia dam kile kisu,,,wakati huo huo akawaambia wachawi wenzake wafumbe macho.
Baada kumalizika Mambo yake,aliwaambia wafumbe macho..
“waoooo….ndege?..” Alisema Makongoro huku akitabasam baada kuiona ndege..
Ruksa ilitoka kwa Mzee Mahulubila..akiwaambia wachawi wenzake waingie ndani ya ndege ile ya kichawi,kwa niaba ya kuelekea gambosh kwenye chimi chimi ya uchawi…….Mzee baluguza alimshika mkono mjukuu wake,,wakazipiga hatua kuelekea ndani ya ndege..wakati huo Makongoro akionekana kuwa na shauku kubwa ya kuipanda ndege ile ambayo ilitokea kimazingala.
Hatimae ndege ile ya kichawi ilipaa angani..wakati huo ikiwa haina sauti yoyote……Na wakati ndege ile ilipokuwa bado ipo angani..Mzee baluguza alimgeukia mjukuu wake ambae msamaha wote alikuwa akitabasam kupanda…Mzee baluguza akasema “huku tunakokwenda…nakuomba uwe makini sana!! ukiona kitu usikikodolee macho sana pia maswali yako ya kipuuzi siyataki..vilevile chakula chochote au kinywaji ukipewa tumia..tofauti na havyo utafia huku huku”
Aliongea hivyo Mzee baluguza..maneno ambayo yalimnyong’onyesha Makongoro akiwa haelewi babu yake anampeleka wapi na pia kufanya nini na japo lile la wachawi..
Wakati Makongoro akiendelea kujiuliza bila kupata jibu,mala ghafla ndege ile ya kichawi ilianza kuyumba yumba..Na punde si punde nyuma ulizuka moto
Moto ule ulienea kwenye ile ndege ambayo ulikua imepakia jopo la wachawi…wakati huo Makongoro alikuwa akipiga kelele kuomba msaada…lakini kelele zake Makongoro zilifikia tamati baada Mzee baluguza kumziba mdomo..wakati huo huo mmoja wa wachawi waliokuwemo ndani ya ile ndege,alionekana kuzipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Mzee baluguza ambae alikuwa akihaha kumziba mdomo mjukuu wake ili asipige kelele.
“Mzee mwanzangu huyu nani yako??…maana anavyo onekana ni mgeni katika safari hizi..” alisema yule mchawi ambae alionekana kuwa na cheo frani katika kazi ile ya kichawi.
“Mmh huyu bwanaaa…ni mjukuu wangu..ila kwa kua kijijini kwetu wamecharuka kutaka kumuangamiza?? hivyo nimeona heri nije nae huku ili na yeye aweze kujilinda dhidi ya maadui zake..” Alijibu Mzee baluguza.
“Anhaa jambo jema Mzee mwenzangu,sina la ziada”
Kwisha kusema hivyo,,hatimae ndege ile ya kichawi ilitua chini…ampapo mkuu wa safari aliinyoshea kidole ndege..ghafla ikageuka kuwa kisu kama ilivyokuwa awali kabla ya kugeuka kuwa ndege.
Wakati huo huo walionekana binadam wawili wa kutisha,,ambao mmoja alikuwa na jicho moja katikati,na mwingine hakuwa na maskio…wote walikuwa wamevaa koti nyeusi ambazo zilikuwa na kofia zake..hivyo watu wale walipiga hatua kuelekea mahali walipokuwa Makongoro pamoja na jopo nzima la wachawi aliotua nao.
“Babu hao ni akinanani??..”
“Shiiiiiii kaa kimya” Alijibu hivyo kwa kunong’ona Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake baada kuulizwa kuhusu wale watu waliokuwa wakiwafuata.
“Karibuni” Wale watu walisema huku wakiambaa kuelekea kwenye jengo kubwa ambalo mlangoni ilionekana nembo ya kichawi..na chini ya hiyo nembo yalionekana maneno ambayo yaliandikwa kwa rugha ya ajabu ajabu…ingawa baada kuingia ndani zaidi,Makongoro aliliona jina gambosh katika koldo moja ndani ya ile nyumba..na hapo ndipo alipo faham kuwa tayali wametua katika ardhi ya gambosh.
Hivyo wale watu walionekana kutisha kwa upande wa Makongoro,walizidi kupiga hatua huku Makongoro na babu yake pamoja na wale wachawi wengine wakiwafuata nyuma…mwishowe walifika katika ukumbi mkubwa ambao ulikua umesheheni watu wa kila aina.
Makongoro walipigwa na butwaa baada kuwaona wachawi wale..alitamani kumuuliza babu yake kisa kilicho wafanya watu wale kufulika kiasi kile katika ile ukumbi,,lakini aliogopa kwa sababu babu yake alisha mkataza kuuliza uliza maswali….Wakati ule ule mbele yake Makongoro..alikiona kiti ambacho kilikuwa kiking’aa mfano wa almasi…Na katika kiti kile,alitokea mtu mmoja ambae kimwonekano alikuwa na jinsi mbili tofauti..kwani hata sauti aliyopasa ilisikika mala mbili,yaani ya kike na yakiume..vile vile yule mtu katika kifua chake alionekana kuvaa cheni zenye nembo ya mafuvu.
Aliogopa Makongoro baada kumwona yule mtu …alitamani kumuuliza babu yake kuhusu yule mtu,,lakini mwendo ule ule alisita baada kukumbuka kuwa babu yake hataki maswali.
Kimya kilitawala katika ukumbi ule..na ghafla ilisikika sauti ndani ya ule ukumbi,,ukumbi ambao ilikuwa umejaza wachawi mbalimbali pamoja na binadam wa kila aina..sauti hiyo ilisema..”Wote simameni na kisha tuungame kabla hatujaanza kuyadadavua masuala yaliyotukutanisha mahali hapa..” Ilisema hivyo ile sauti..sauti ambayo ilisikika katika jinsia mbili,ya kike na ya kiume…
Hivyo wachawi wale walifanya kama amli ilivyosikika…kasolo Makongoro ambae hakusimama ingawa nae alishikwa mkono na babu yake akimtaka asimame kama wengine walivyo fanya…
Baada kumalizika kuungama..wot kwa pamoja walikaa chini..na hiyo ikawa nafasi pekee ya Makongoro kutazama kila pande katika ukumbi..akiwa bado katika kutazama tazama,,mala ghafla alishtuka baada kumwona mwalimu wake wa hisabati ambae aliitwa shija..nae akiwa miongoni mwa wachawi waliokuwemo ndani ya ule ukumbi..Makongoro alijiuliza ni vipi mwalimu wake atoke Dar es salaam ambako anafanya kazi,moja kwa moja aonekane gambosh?? Na hapo ndipo Makongoro alipokumbuka kuwa mwalimu huyo alishahusishwa na tuhuma za kichawi,,ila zikawa zimeishia chini chini….na hivyo Makongoro akawa amefaham kuwa mwalimu shija ni mchawi kama alivyokuwa akituhumiwa na wanafunzi wa shule mwenge..shule ambayo mwalimu hiyo alikuwa akifundisha pia Makongoro nae akiwa miongoni mwa wanafunzi wa shule hiyo.
Makongoro aliduwaa huku akimtazama vizuri mwalimu yule…wakati huo huo shija nae aligeuka upande aliokuwa Makongoro…na hivyo wakawa wamekutana uso kwa uso…kitendo ambacho kilimfanya shija kurudisha uso wake kama awali baada kumwona Makongoro ambae alikuwa ni mwanafunzi wake “Mmh huyu Makongoro kafikaje fikaje huku??.. na bila shaka atakuwa kanijua…na kama kweli kanijuwa,,hakika nitafanya juu chini ili nimwangamize kabla unga haujazidi maji” Alisema shija baada kuingiwa na hofu kuhusu Makongoro.
Na wakati hayo ya Makongoro pamoja na mwalimu wake ambae ni shija…alipokuwa yakiendelea,upande wa pili nako yule mtu mwenye jinsi mbili tofauti…aliendelea kuzungumza Mambo mbalimbali kadha wa kadha..na katika mambo hayo ilikuwemo suala nzima la kugawa uchawi kwa watakao hitaji..kisha akaomba majina ya watu wanao hitaji na aina gani ya uchawi unaotakiwa.
Kwisha kusema hayo kengere ililia,,kuashilia kuwa umefika muda wa kula chakula…hivyo mtu yule ambae alikuwa akiendesha Mkutano ule wa kichawi..aliwaruhusu wachawi wake wakale Kwanzaa chakula kisha waendelee na Mkutano..ambapo Mzee baluguza alimshika mkono mjukuu wake,moja kwa moja walielekea kwenye chumba mahususi kwa kulia chakula..Chumba ambacho kila kona ilisikika harufu ya dam za binadam.
“Chochote utakacho letewa kula wala usiohope…na pia ukienda kuchukuwa uchawi kwa yule kiumbe,,Naomba uchukuwe uchawi wa kujilinda na kuua..Sarawak??..” Mzee baluguza alimwambia hivyo mjukuu wake kwa msisitizo… huku wakiwa tayali wameketi kwenye viti ambavyo vilitengenezwa kwa kutumia mifupa binadam pamoja na ngozi ya Chui..
Hivyo Makongoro baada kuambiwa vile na babu yake,aliitikia kwa kichwa..wakati huo huo alionekana binti mzuri ambae miguu yake ilikuwa kama mbuzi..binti yule akiwa na bakuli mbili mkononi,,alizipiga hatua kuelekea kwenye meza ambayo walikuwa wapo Mzee baluguza pamoja na Makongoro.
Hivyo binti yule baada kuifikia meza ile..aliwapa zile bakuli baluguza na mjukuu wake…ampako Mzee baluguza aliufakamia kwa pupa mchuzi uliokuwemo ndani ya bakuli yake….wakati huo Makongoro nae alipo ingiza kijiko chake kwenye mchuzi katika bakuli lake…ghafla alistisha baada kuona kiganja cha macho ya binadam yakielea kwenye ule mchuzi.
“Lazima ule la sivyo hutoki huku…”
Alisema Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake…baada kumwona akiogopa kuyala yale macho ambayo ni chakula maalum kilicho andaliwa kwa niaba ya wachawi watakao hudhulia Mkutano gambosh.
Makongoro aliyatazama yale macho yaliyokuwa yakielea kwenye mchuzi ndani ya bakuli..kisha akamtazama na babu yake ambae alionekana kula chakula kile bila wasiwasi…ghafla mate yalimjaa Makongoro mdoni,,akahisi kichefuchefu….na punde si punde alitapika..kitendo ambacho kiliwafanya wachawi wote waliokuwemo ndani ya chumba kile kusimama huku wakikodele macho meza ambayo alikuwa kakaa Mzee baluguza na mjukuu wake ambae ni Makongoro.
“Nani huyo ambae anafanya ujinga hum ndani??..” Mchawi mmoja mwenye ulemavu wa ngozi yaani albino..alisikika akisema hivyo kwa sauti kali..ambapo hapo hapo,alionekana mchawi mwingine alinyoosha kidole kuelekea kwenye meza ambayo aliketi Mzee baluguza nammjukuu wake.
Hivyo baada mchawi yule albino kuonyeshwa ,,haraka sana alizipiga hatua kuelekea kule alikokuwa Mzee baluguza…wakati huo Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake kwa sauti ya kunong’ona..akisema “Unaona sasa tayali umeshavuruga…tangu awali nilikwambia chochote utakacho letewa we kula tu hata kwa kujikaza ili ufuzu zoezi la kupata uchawi !! Lakini wewe unajifanya mtoto wa mjini,,haya sasa kazi kwako..huyooo albino anakuja”
Alisema hivyo Mzee baluguza huku akiangalia jicho ngembe kule anakutokea mchawi albino.. Makongoro aliogopa,hima alinyanyuka kutoka kwenye kiti akitaka kumkimbia mchawi albino..lakini Mzee baluguza alimtuliza kwa kumwambia kuwa “endapo ukikimbia basi utakufa” Makongoro baada kusikia neno hilo kutoka kwa babu yake..woga ulizidi maladufu..akajikuta yupo Kati kwa Kati,kukaa alishindwa pia kukimbia alishindwa…Hivyo alisimama huku akitetemeka,na macho yake yakimtazama mchawi albino ambae nae alizidi kuzipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Mzee baluguza na Makongoro.
Baada mchawi albino kufika katika meza ile ya Mzee baluguza..ghafla alimshika Makongoro kisha akavuta kwake kwa nguvu…huku akiongea rugha ambayo Makongoro na babu yake hawakuweza kuielewa…
Hakika Makongoro alipasa sauti ya kilio..akiomba msaada asaidiwe..lakini cha ajabu wachawi wote waliokuwemo ndani ya kile chumba akiwemo Mzee baluguza..hakuna aliejitolea kumng’atua Makongoro katika mikono ya yule mchawi albino ambae alionekana kutaka kumuua Makongoro.
Hivyo wachawi wote waliishia kutazama tu..wakati huo minong’ono mbili mbili ikisikika kwa chini chini..minong’ono ambayo ilisikika ikimsifu mchawi yule albino kwa uhodari aliokuwa nao wa kupigana kichawi….wakati huo Mzee baluguza yeye alikuwa ameweka mikono kichwani akitazama jinsi mjukuu wake alivyokabwa na mchawi albino…kwa hakika alimwonea huruma sana,,alitamani kwenda kumwokoa..lakini Mzee baluguza akajikuta kuwa nguvu alizo nazo hawezi kupigana na mchawi albino..mchawi ambae alibarikiwa nguvu aina Saba za giza.
Lakini wakati mchawi yule albino,alipokuwa akiendelea kukazana kutaka kumtoa roho Makongoro..mala ghafla katika wachawi wale therathini waliosafiri na Makongoro kutoka sumbawanga mpaka gambosh..alijitikoze mmoja ambae alifahamika kwa jina gwimo..ambapo gwimo kwa kutumia kiganja chake aliunyoosha mkono wake kisha akampiga moto mchawi albino..nae baada ule moto kumpata,haraka sana alimwachia Makongoro..kisha akamgeukia yule aliempiga moto wa kichawi.
Hivyo akionekana kughadhibishwa na kitendo kile..mchawi albino aliongea tena maneno yasiyoeleweka..lakini hakujibiwa na mtu..zaidi gwimo alijitokeza na kisha kusemama “Mimi hapa gwimo mwana wa gwimo” Kwa kauli ya kishujaa kabisa mchawi gwimo alijigamba mbele ya mchawi albino..ambae alikuwa si mchezo katika shunghuli nzima ya kupigana kichawi.
Wakati Mzee baluguza akimnyoosha mjukuu wake shingo baada kutoka kwenye imaya ya mchawi albino…upande mwingine nako walionekana wachawi baadhi wakisogeza meza kando ili kuwaachia nafasi mchawi gwimo na mchawi albino..ambae tayali alikuwa amesha badilika uso kutoka katika umbile la kibinadam..na kuingia katika umbile lingine tofauti..maskio yake yalipotea huku macho yake nayo yakionekana kuwa kama ya nyoka.
Wakati huo gwimo yeye hakubadilika kitu chochote..zaidi aliikaza vizuri kiunoni vazi lake nyeusi..kisha akasimama katikati ya uwanja..ambapo mchawi yule albino aliasama mdomo wake..ghafla ulitoka moto mkali uliomfuata gwimo ..lakini kwa kuwa gwimo nae hakuwa haba..hivyo aliweza kuukwepa moto ule.
Hakika shangwe za kumshangilia gwimo..zilisikika baada kupangua moto ule .na pia ziliongezeka maladufu baada gwimo kujibu shambulizi ambalo moja kwa moja lilimkuta mchawi albino..ambapo alianguka chini mfano wa mzigo wa kuni utokapo kichwani.
Kwa hasira kali mchawi albino alinyanyuka akata kujibu shambulizi..lakini ghafla kengere ililia kuashilia kuwa muda wa kurudi ukumbini umewadia..na hivyo mchawi yule albino alirudi katika hali yake ya ubinadam..kisha wakaelekea ukumbini..wakati huo Mzee baluguza akiwa sambamba kabisa na mjukuu wake Makongoro..ambae nae baada kunusurika kifo kutoka kwa mchawi yule katili albino,alitamani akalipe kisasi kwanza pindi atakapo pewa uchawi.
Hivyo mala baada kufika ukumbini..ghafla ilisikika sauti ya mkuu wa wachawi ikiwata wale wachawi waliokuwa wakipigana watoke nje wakalishe misukule..mpaka pale kikao kitakapo kitakapo malizika..ambao watu hao ni mchawi albino pamoja na mchawi gwimo.
Wote walinyanyuka kila mmoja akimtamani mwenzie,,kisha wakapotea pale kwenye kikao..ambapo baada kupotea kwa hao wachawi..punde punde mkuu yule wa wachawi gambosh..aliwataka chipkizi wanao hitaji uchawi…….Hivyo haraka sana Mzee baluguza alirudia kumkubusha Makongoro..akisema “Tafadhali nakuomba uchague uchawi wa kuua na kujirinda dhidi ya maadui sawa sawaa” Aliaisitiza Mzee baluguza..wakati huo Makongoro akiwa tayali kanyuka..hivyo alizipiga hatua kuelekea kwa mkuu wa wachawi,,hakuwa peke yake bali alikuwa na chipkizi wengine mbalimbali wiliotoka mataifa tofauti tofauti ndani na nje ya bara la Africa.
Na baada Makongoro na wenzake kufika kwa mkuu yule wa wachawi..hatimae aliondoka nao moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha kiapo..ambapo katika chumba hicho zilisikika sauti mbalimbali za wafu pamoja na harufu mbaya iliyoenea chumba kizima..Hakika Makongoro aliogopa sana,,ila aliamua kupiga moyo konde,na hivyo punde si punde ilisikika sauti nzito ndani ya kile chumba cha kiapo..saut ambayo ilisikika ikisema “kabla ya kuapa..lazima ule kwanza nyama mbichi ya binadam pamoja na kikombe cha damu..kwani hicho ndicho chakula chetu stahiki kama ilivyo wali kwa mwanadam wa kawaida”
Kwisha kusema hivyo..ghafla mbele yake Makongoro alitokea mtu alievaa koti jeusi kuanzia juu mpaka chini,,,,akamkabidhi Makongoro bilauli kubwa lililokuwa limejaaa ulimi na sehem ya Siri ya mwaume pamoja na moyo bila kusahau kikombe kikubwa kilicho sheheni damu nzito ya binadam.
Makongoro alizitazama zile nyama..ambazo zilikuwa zikitoka dam wakati wote..Hakika alijutia kwanini aliamua kwenda kumtembelea babu yake kijijini..maana laiti kama ningebaki zake mjini,basi hayo mambo yote yasingemkuta…Hivyo Makongoro akiwa ameyafumba macho yake..alikula zile nyama mbichi moja baada ya nyingine..na baada kumaliza alishushia na damu nzito iliyokuwa kwenye kikombe..wakati huo huo kwa mbali zilisikika sauti za watoto wakishangilia,,,sauti ambazo Makongoro hakuweza kutambua mahali zinapotokea.
Na Makongoro alipokuwa akiendelea kustajabishwa na zile sauti za watoto..mala ghafla mbele yake alitokea mkuu wa kichawi huku akiwa na jungu kubwa lililokuwa likifuka moshi mweusi…mkuu yule alitabasam baada kumwona Makongoro kafuzu mtihani wa kula nyama mbichi..hivyo moja kwa moja alimwamlisha anyooshe mkono wake,,nae Makongoro alifanya hivyo hivyo…ambapo mkuu yule wa wachawi alimshika mkono,kisha akasema
“Unaitwa nani..??”
“Makongoro..”
“Anhaa jina nzuri sana kijana..pia nikupe pongezi ya kufaulu huu mtihani mzito,,kwa Hakika wewe ni jasiri kupita kipimo na nakutabilia kwa siku za usoni wewe utatisha bala nzima la Africa….Lakini yote kwa yote..napenda Nikuulize maswali tofauti tofauti..na katika kujibu tamka neno..ng’onilo sawa kijana??..”
“Sawa” Aliitikia Makongoro hivyo huku akijifuta baadhi ya mabaki ya damu katika mdomo wake.
Na hapo ndipo mkuu yule wa wachawi alipo anza kumuuliza maswali mbalimbali Makongoro…na kati ya maswali hayo aligusia jinsi gani kijana ataweza kuilinda na kuiheshim kazi yake ya kichawi…nae kwa kujiamini Makongoro alijibu “Ndio nitailinda na kuiheshim”…Baada Makongoro kujiibu vizuri,ghafla kilitokea kitabu kikubwa kwa mkuu yule wa wachawi..na muda huo huo ulitokea msukule..msukule ule ulizipiga hatua mpaka kwa mkuu wa wachawi kisha akainama chini..ambapo uliweza kugeuka kuwa meza.
Hivyo mkuu yule wa wachawi akawa amekiweka kitabu juu ya mgongo wa msukule ambao umegeuka kuwa meza..kisha akamwita Makongoro ili asaini..Makongoro nae kwa kua kila kitu kigumu alikuwa ameshakivuka,,Hakika hakusita kwenda kusaini..alisaini kwa kujiamini kabisa..kwani baada kuinywa damu ile ya binadam nafsi yake iliingia dosari kidogo..dosari ya kutokuogopa kitu.
Na wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako..alionekana mchawi albino na mchawi gwimo wakizozana…badala ya kufanya kazi waliyopewa ya kulisha misukule kama moja ya adhabu waliyopewa na mkuu wao wa wachawi,,baada kuonekana wamegombana kinyume na sheria ya gambosh…hatimae walijikuta wakirudia kupigana..ambapo mchokozi alikuwa ni mchawi albino ambae hapo awali alionekana kuzidiwa uwezo na gwimo licha ya yeye kusifika kwa uhodari wa kupigana kichawi zaidi…hivyo lengo la mchawi albino ni kutaka kumnyoosha gwimo ili atunze heshima yake katika kijiji kile cha gambosh.
Hakika patashika nguo kuchanika mapigano ya nguvu yakiendelea katika nyumba ile ya kutunzia misukule..wakati huo misukule nayo ikilia njaa kiasi kwamba ilivunja milango na madirisha..kisha ikasambaa sehem mbalimbali..Huku ugomvi wa mchawi albino na gwimo bado ukiendelea kupamba moto,pasipo kujuwa kuwa wamesababisha balaa la misukule kutoroka.
Na ugomvi ule ilipokuwa ukiendelea…Kwingineko nako..mkuu wa wachawi alionekana kumkabidhi Makongoro hirizi tisa zenye ukubwa tofauti tofauti kisha akaondoka nae moja kwa moja mpaka kwenye Mkutano..ambapo alikuta maongezi mbalimbali yakiendelea katika ukumbi ule wa wachawi..na hivyo baada mkuu kutokea,hatimae kimya kizito kilitawala huku wachawi wale wakijiuliza chipkizi wengine wako wapi mpaka mkuu arudi na chipkizi mmoja ambae ni Makongoro..lakini maswali yao kabla hawajayapatia majibu,,mala ghafla mkuu yule wa wachawi alipasa sauti akisema “Kwanza kabla ya yote,,ebu mpongezeni kijana huyu Mdogo kwa kile alicho kifanya..kwa Hakika huyu ni kijana jasiri natumai siku za karibuni atatisha sana” Alisema mkuu yule wa wachawi..ambapo hapo kelele za wachawi wakimpongeza Makongoro zililindima kila kona ya ukumbi..ila kasoro mtu mmoja tu hakuweza kumpongeza Makongoro..ambae nae si mwingine ni mwalimu shija…
Hivyo mala baada pongezi kumfikia Makongoro..hatimae mkuu yule wa wachawi alielezea aina ya chakula alichopewa Makongoro kama moja ya mtihani.. Hakika wachawi wote walibaki midomo wazi…wakati huo Mzee baluguza akimtazama mjukuu wake na kisha kusema “Inaamna supu ya macho mbaya..ila nyama mbichi tena ya sehem ya Siri ndio tamu??…Hahahaaaaa kweli mjukuu ninae..pole yao Mzee mwakipesile” Hakika Mzee baluguza alisema hivyo huku akiachia tabasam pana.
Hivyo baada ya hayo mkuu wa wachawi..alitaka kufunga kikao..lakini kabla hajafunga,ghafla Bibi mmoja alietokea nchini Congo ambae nae alimpeleka mjukuu wake gambosh ili apewe uchawi..alisimama na kisha kuhoji mahali alipo mjukuu wake pamoja na wenzake..
“Wameshindwa mtihani..kwahiyo sheria yetu inasema mtu yeyote akiferi mtuhani..hastahili kurudi katika jamii ya watu wa kawaida kwa maana atavujisha Siri” Kwa sauti Kali…mkuu yule wa wachawi alimjibu bibi kizee…ambapo nae baada kusikia maneno hayo aliangua kilio kikubwa huku akilitaja jina lamjukuu wake..
Wakati huo huo mkuu yule alifunga kikao kisha akatoweka..
Na baada mkuu wao kuondoka!?..Mzee baluguza alizipiga hatua kumfuata mjukuu wake alietunukiwa jopo la hirizi na uchawi wa kutosha…hivyo moja kwa moja walijikusanya pamoja kama walivyotua katika ardhi ya gambosh..lakini kati yao alipungua mmoja ili watimie therathini …ambae ni gwimo..kwahiyo haraka sana harakati za kumtafuta zilifanyika..lakini hakuweza kumpata..na hivyo mkuu wa msafara alichukua kisu chake kidogo..ambapo kufumba na kufumbua kiligeuka kuwa ndege..wote walipanda hatimae safari ya kurudi Tanzania ikaanzaa baada kukaa gambosh kwa siku mbili……Hivyo ndege ile ya kichawi baada kufika sumbawanga ilitua chini..ambapo walishuka Mzee baluguza na mjukuu wake kisha kila mmoja akachukua ungo..na safari ya kurejea kijijini bhonde iliendelea,,wakati kijiji kilikuwa kimechafuka wakimtafuta Mzee baluguza kwa udi na uvumba ili wamuuwe baada kugundulika kuwa yeye ndio alie husika na kifo cha mama chiku..mama muuza pombe alieuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na Mzee baluguza..wakati huo huo Mzee kinono nae alikuwa akimuwinda Makongoro ili amteketeze.
Mzee baluguza akiwa na mjukuu wake ndani ya ungo wakirudi kijijini baada kutoka gambosh..ghafla walishtuka walipoona moto ukiwaka kwa mbali katika kijiji chao cha bhonde…hivyo moja kwa moja Mzee baluguza Alimtazama mjukuu wake ambae alikuwa pembeni yake kidogo,kisha akasema “Makongoro jiandae,,maana moto ule unao uona si bure”
Alisema Mzee baluguza huku akijifunga vizuri hirizi yake kwenye mkono wake…ambapo nae Makongoro alifanya hivyo hivyo…na baada ya dakika kadhaa,walitua chini nje kidogo na nyumba yake Mzee baluguza…ambapo baluguza na mjukuu wake,kwa pamoja walichuchumaa style ya kupiga magoti mfano ya wanariadha,,punde si punde walipotea nje,wakatokea ndani.
Hakika kitendo kile kilimfrahisha sana Makongoro…akajikuta akitabasam huku akimtazama babu yake,ambapo nae Mzee baluguza aliachia tabasam kama vile alivyofanya mjukuu wake,kisha akasema “Naam Makongoro kazi nzuri…Sasa kama wanajiamini wachokoze moto huu” Alisema Mzee baluguza akionekana kujiamini kabisa.
“Hahahaaa babu bwanaa sawa mimi niko sawa kila idara” Makongoro alijibu hivyo huku akipiga kifua chake kuonyesha kuwa yupo sawa kwa lolote kwa chochote.
“Sawa mjukuu wangu nenda kalale ila kumbuka kesho pasaka,,hivyo mchana tutajumuika pamoja kufrahia sikukuu,ila usiku tutaelekea buharamulo kwenda kula chakula chetu cha kichawi”
“Sawa babu nimekuelewa..usiku mwema” Makongoro alimjibu babu yake kisha akaingia chumbani kwake.
Wakati hayo yakiendelea,upande ule ambako ilionekana moto..walionekana wachawi wa kijiji cha bhonde wakiimbana kucheza huku wakiwa uchi,,wakati huo pembeni yao likionekana jungu kubwa lililokuwa limejaaa nyama za binadam likiwa juu ya mafiga…hivyo baada kuimba na kucheza kwa muda mrefu,hatimae mkuu wa hafra ile ya kichawi alistisha ngoma kisha akasema “Jamani tumefrahi vya kutosha..tukiimba na kucheza ila kwa sasa ni muda wa kula kitoweo kilicho andaliwa mahususi kwa siku ya leo” Kwisha kusema hivyo mkuu yule wa hafra ambae aliitwa Mzee dole tupu,,ghafla kelele na moyowe ya wachawi zilisikika kila pande…huku mirunzi kadha wa kadha nayo ikifuatia…bila shaka hiyo yote ilikuwa ni furaha ya kusikia jina kitoweo.
Mkuu wa hafra alimteua Mzee sule ndio awe mgawaji wa chakula…hivyo Mzee sule aliweza kuifanya kazi ile kwa umakini zaidi..nacho chakula kile zilikuwa ni nyama za binadam.
Baada wachawi wale walipomaliza kula chakula chao,,hatimae mkuu wa hafra aliwataka waondoke majumbani mwao…lakini kabla hawajasambaa,mala ghafla alikuja popo katika sherehe ile..popo huyo alitua moja kwa moja kwenye bega la Bi kileleganya ambae muda wote mwanzo mpaka mwisho wa sherehe alikuwa kakaa pembeni akiwatazama wachawi wake jinsi wanavyo frahia sherehe..
Hivyo baada popo yule kutua kwenye bega la Bi kileleganya….hima alisimama kisha akasema “Natumain wote kwa pamoja mmefurahi sana..lakini furaha yenu hii isiwafanye mjisahau kujilinda..” Alisema Bi kileleganya kisha akameza mate..lakini kabla hajaendelea,mala ghafla ilisikika sauti ya mmoja ya wachawi,,sauti hiyo ilisikika ikisema ” Unamaana gani mkuu” Kwisha kusema hivyo yule mchawi..wachawi wenzake walimtazama kwa jicho baya..huku kwa kunong’ona ilisikika sauti nyingine ikimjibu “We kaa kimya..usirudie tena kuongea wakati mkuu hajamaliza kuongea” Alionywa hivyo yule mtu..ambapo nae aliomba radhi huku akionekana kuwa na hofu..lakini Bi kileleganya,licha ya kuisikia ile sauti..ila hakuweza kudili nayo kwani alijuwa ni presha iliyomkamata mchawi wake…hivyo aliendelea na kitu alichotaka kuongea..” Jamani naombeni nisiwachoshe…ila ninacho wataka ni nyinyi kuwa makini..maana Mzee Baluguza karudi…” Alisema kwa msisitizo Bi kileleganya huku akiwakodolea macho wachawi wake..ambao nao walionekana kupigwa na butwaa baada kusikia jina Baluguza.
Na wakati wachawi wale wakiwa katika dimbwi la wasiwasi…mala ghafla Bi kileleganya alimwita Mzee mwakipesile,kisha akamwambia ” Mwakipesile fanya kazi yako sasa ya kutuletea yule mjukuu wa Mzee baluguza kwenye familia yetu..Sawa sawaa??..”
“Sawa mkuu…” Kizee mwakipesile alijibu kwa heshima..
“Haya mnaweza kurudi majumbani kwenu” Aliongeza kwa kusema hivyo mkuu yule wa wachawi kijijini bhonde..ambapo yeye ndio alikuwa wa kwanza kupotea maeneo yale,,kisha wengine wakafuatia..punde si punde wote walipotea.
Usiku uleule kabla hapajakucha…Gambosh nchini Nigeria..Mchawi albino na mchawi gwimo..walijukuta wakiwa katika wakati mgumu baada kukutwa wakigombana…wakati huo wakisababisha misukule kutoroka.
Katika chumba mahususi kwa niaba ya mateso..walipelekwa wachawi wale..lakini kwa kuwa mchawi albino alikuwa akijiamini kwa sababu ya kuwa na nguvu nyingi za giza,hatimae alipinga mateso ambayo angeyapata..kitendo kilicho mkera mkuu wa kitengo cha mateso..ambapo aliamulu kuwa mchawi albino abebe naaadhabu ya gwimo….hivyo gwimo nae alibadishiwa adhabu..ambapo alipelekwa shambani kulima.
Hakika gwimo alilima sana siku hiyo…istoshe alipokonywa nguvu zake za kichawi…hivyo akawa analima yeye kama yeye..
Wakati huo katika chumba kile cha mateso ilikuwa patashika nguo kuchanika,,ugomvi Kati ya mchawi yule albino na mkuu wa kitengo cha mateso…kwani mchawi albino alionekana kupinga mateso,,na hivyo ikawa imefikia hatua ya kupigana…..Lakini wakati wakiwa katika mapigano,,mala ghafla alitokea mkuu wa wachawi Africa nzima…Mkuu yule alionekana mifupa tu bila ngozi wala nyama za mwili..ambapo mkuu yule wa wachawi kwa kutumia rupia yake aliyokuwa nayo mkononi…aliizungusha kwa kuipitisha katikati ya vidole vyake…wakati huo mchawi albino alikuwa akiishiwa nguvu kila sekunde zilivyozidi kwenda…mwishowe kabisa akinyong’onyea kabisa..ambapo alifungwa nyororo kisha akavuliwa nguo mwili mzima..na punde si punde baada kufungwa mnyororo,ghafla alitokea mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano..mtoto yule alizipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa mchawi albino akiwa katika fundo za nyororo..Hivyo baada kumfikia…mtoto yule alinyoosha mkono wake juu..punde si punde Katika mkono wa yule mtoto ilitokea bakuli kubwa na mkasi mdogo mkali…..mtoto yule alicheka kwa sauti Kali iliyoambatana na mwangwi mkali,,na mala baada kumaliza kucheka,aliuchukua mkasi kisha akaanza kukata kiungo kimoja baada ya kingine kwenye mwili wa mchawi albino,,ambae nae alipasa sauti Kali ya kuhisi maumivu.
Wakati huo kijiji bhonde..wachawi wote waliingiwa na hofu baada kusikia habari za Mzee baluguza…lakini hali hiyo ilikuwa tofauti kwa Mzee kinono..kwani baada kusikia kuwa Mzee baluguza karudi,haraka sana alichukua ungo wake,kisha akapaa kumfuata nyumbani kwake kwa lengo la kwenda kumuuwa Makongoro..mjukuu wa Mzee baluguza..pasipo kujuwa kuwa Makongoro nae kapewa uchawi.
Angani saa za usiku..alionekana Mzee kinono akiwa ndani ya ungo akisafiri kumfuata Makongoro kwa nia ya kulipa kisasi…kwani ikumbukwe kuwa Makongoro alimpa paka jiwe,,pasipo kujuwa kuwa paka yule alikuwa ni mtoto wa Mzee kinono..Na Hivyo kitendo kile kilimkela sana Mzee kinono,,mpaka akaamuwa kujenga chuki dhidi ya Mzee baluguza ambae ni babu yake Makongoro.
Lakini kabla Mzee kinono hajatua kwenye nyumba ya Mzee baluguza,,mala ghafla ungo wake uliyumbishwa..Mzee kinono alishtuka baada kuona hali ile..Hivyo alichukua kibuyu chake kidogo alichosafiri nacho,pia akachukua na kipisi cha mkia wa ng’ombe..ambapo mkia ule aliuchovya kwenye kile kibuyu chake kilichokuwa na damu kisha akanyunyuzia kila pande kuu ya dunia.
Na mala baada Mzee kinono kufanya hicho kitendo…haraka sana alifungua mkoba wake chakavu,kisha akatoa hirizi kubwa,,hirizi hiyo alijifunga kwenye mkono wake huku akiongea maneno ya kichawi….ambapo punde si punde ungo ulitulia.
“Mimi ndio mfalme wenu pumbafu zenu” Alijigamba hivyo Mzee kinono baada kufanikisha kuutuliza ungo wake kwenye ramani sahihi..wakati huo kwa mbali walionekana wachawi wengine wakielekea kule alikitoka Mzee kinono,,lakini cha ajabu wale wachawi waligeuka na kisha kumfuata Mzee kinono kwa kasi ya ajabu..
Kwa hakika Mzee kinono nae baada kujishtukia kuwa anafuatwa na wachawi nyuma yake..hima nae aliongeza kasi ili kuwakimbia wale wachawi ambao walionekana kuwa na uwezo mkubwa kuliko yeye.
Hivyo wakati hayo yakiendelea…upande mwingine nako Makongoro nae alipokuwa amelala kitandani..mala ghafla alishtuka kutoka usingizi baada kusikia sauti ikimwita…..sauti hiyo haikuwa ya mtu mwingine bali ilikuwa sauti ya mkuu wa wachawi..ambapo Makongoro baada kuifaham ile sauti aliondoa hofu mwili,alisimama kando ya kitanda chake kisha akakaa tayali kumsikiliza mkuu wake anasemaje,,
Na wakati Makongoro alipokuwa kimya,,akimsikiza mkuu wake ili aseme neno..ghafla chumbani kwake ulitokea mwanga mkali…mwanga huo kabla haujatoweka mle chumbani..ulitokea mkono bila kiwiliwili,mkono huo ulikuwa umeshikilia hirizi ukimpatia kijana Makongoro.
Makongoro bila wasiwasi aliizipiga hatua kuifuta ile hirizi…Na mala tu alipo ishika ..sauti ya mkuu wa wachawi ilirudia kusikika ikisema “Makongoro hiyo ndio kila kitu kwako..Sema kitu chochote cha kichawi utakipata…Hivyo itunze itakusaidia” Kwisha kusema hivyo..ile sauti ilipotea,na mwanga ule mkali nao ulizimika..ambapo Makongoro nae alijifunga vizuri ile hirizi kwenye mkono wake kisha akarudia kitandani kulala..
Ils la kabla usingizi haujamkamata..ghafla ile hirizi aliyokuwa ameivaa mkononi ilianza kumbana kiasi kwamba akashindwa kulala..akawa amekaa kitandani tu….Na wakati huo huo. Mzee kinono tayali alikuwa ameshatua kwenye nyumba ya Mzee baluguza..ambapo baada kutua..Makongoro akiwa chumbani kwake alisikia mshindo,hivyo alisimama kutoka kitandani kisha akachukuwa nguo yake nyeusi ambayo alijifunga kiunoni..na moja kwa moja alizipiga hatua kuelekea kwenye kona ya chumba chake kisha..punde akawa amepotea akatokea nje.
Mzee kinono baada kumwona Makongoro alicheka sana kwa dharau na kejeli,,na baada kumalizika kucheka alisema “Eti na wewe unatuiga sisi??..sasa acha nikionyeshe ili utambue kuwa uchawi na ugolo ni vitu viwili tofauti” Alisema Mzee kinono akimaanisha kuwa Makongoro hana uchawi,bali anaugolo kwa sababu ugolo na uchawi vinafanana.
Hivyo Mzee kinono baada kusema hayo alirusha kombola moja la kichawi kuelekea mahali alipokuwa Makongoro..lakini cha ajabu Makongoro alipotea akatokea nyuma yake Mzee kinono..kitendo ambacho kilimshangaza sana Mzee kinono kwa uwezo ule aliouonyesha kijana Makongoro.
Ila licha ya Mzee kinono kushangazwa na uwezo ule wa Makongoro..kwa Hakika hakutaka kushindwa,,zaidi aligeuka nyuma yake alipokuwa amesimama Makongoro ambae nae alikuwa akicheka mfano wa mtu anaetekenywa.
Na mala baada Mzee kinono kumgeukia Makongoro..safari hiyo hakumrushia kombola,bali alimrushia moto wa kichawi..lakini moto ule kabla haujampata Makongoro..ghafla Makongoro aliunyoosha mkono wake wa kushoto uliokuwa na hirizi aliyopewa gambosh…punde si punde moto ule alio urusha Mzee kinono uliganda kisha ugeuzwa ukawa maji.
“Mmmh” Mzee kinono aliguna asiamini kama kweli Makongoro ndio anaeyafanya Mambo yale..wakati huo akijiandaa kumkimbia kabla kijana hajajibu mashambulizi.
Na haikuchukuwa muda Mzee kinono alipotea akatokea nyumbani kwake. ..ambapo baada kufika,moja kwa moja alichukua jungu lake lililokuwa na makorokoro ya kichawi kisha akaenda nalo mpaka sebleni kwake huku akijiuliza “mtoto yule uchawi mkali vile kautoa wapi??..Daah hapana mimi kinono bwana miaka dahali nipo kwenye uchawi,sasa iweje mtoto mdogo kabisa anishinde??…
ITAENDELEA
Sehemu Ya Nne (4)
“
Wakati Mzee kinono akifanya yake huku akijiuliza kuhusu Makongoro,ghafla mwanae ambae aliitwa Sudi aliamka..alishtuka baada kumwona baba yake akiwa bize na jungu lake la kichawi,kwani alihisi kuwa kimenuka kijiji.. maana Sudi alikuwa ameshakalili kuwa endapo akimwona baba yake ameshika chungu chake,basi lolote limetokea aidha litatokea.
“Sudi..” Aliita Mzee kinono kwa jazba.
“Naam baba.”
“Ebu kuja hapa”
Kwa wasiwasi wa hali ya juu,Sudi alitii wito wa baba yake.
“Mmmh unamfaham yule mjukuu wa Mzee baluguza??. ” Kinono alimuuliza mwanae kwa hisia Kali.
“Mjukuu wa Mzee baluguza??…Ee ndio namfaham si yule alienipiga jiwe siku ile”
“Eeeh huyohuyo…ambae anajifanya yeye mjanja eti kisa ametoka mjini…ila tuachane na hayo,nilichokuitia ni kwamba popote utakapo muona..Tafadhali usimchokoze sawa Sudi??..”
“Sawa baba” Aliitikia Sudi ili kumlidhisha baba yake,lakini ndani ya nafsi yake bado alitamani akutane na Makongoro ili amfanyie mambo.
Baada Mzee kinono kumwonya mwanae kwa Makongoro..hatimae aliendelea na kazi yake ya kuangalia kitu alicho nacho Makongoro…ambapo mwishowe Mzee kinono aligundua kuwa Makongoro anahirizi kubwa na yenye nguvu nyingi..Alicheka Mzee kinono kisha akasema “Mimi ndio kinonoooo..nimesha sema siwezi kusumbuliwa na mtoto mdogo…” Alisema hivyo Mzee kinono huku akipiga kifua chake.
“Sudi mwanangu..”
“Naam baba…”
“Njoo unafanya nini huko..”
“Nachimba mihogo hapa nyuma ya nyumba..ili nichemshe”
“Anha njoo kwanza..” Sudi alitupa jembe chini kisha akatii wito wa baba yake ambae nae alikuwa akiimba nyimbo za kirugha huku akiyumbisha kichwa chake akikipeleka kulia na kushoto..
“Ndio baba nimekuja..”
“Saw sawa…umesema unachimba mihogo kwani Bukulu hayupo??..” Alihoji Mzee kinono..Bukulu ni msukule ambao aliufuga mzee kinono.
“Yupo baba lakini…”
“Lakini nini???…..Acha ujinga Bukulu yupo hapa kutufanyia kazi sawa??”
“Sawa baba nimekuelewa..”
“Naam vizuri sana….pia nakupa taarifa kuwa kisho mimi naelekea mindu kuna dawa frani naifuatilia..Hivyo jukum lako ni kumlinda Bukulu asitolike pia kama nilivyo kwambia kaa mbali na mjukuu wa Mzee baluguza..”
Alisema hivyo Mzee kinono..ambapo aliamua kuanzisha safari ya kwenda mindu kufuata uchawi mwingine mkali ili aweze kumwonyesha Makongoro kuwa ukubwa dawa.
Na wakati hayo ya Mzee kinono yakiendelea..tayali palikuwa pamekucha,,sauti za ndege zilisikika…kijiji cha bhonde kilionekana kuwa tulivu…Na kwa mbali alionekana kijana Makongoro akiwa na bibi yake wakielekea shamba huku wakiongea maneno kadhaa wa wa kadha ..
Lakini wakati walipokuwa njiani,ghafla nyuma yao alitokea Mzee mwakipesile moja kwa moja Mzee huyo alizipiga hatua kuwafuata Makongoro na Bi Mazoea ambae ni bibi yake Makongoro.
Hivyo baada kuwafikia,aliwasalimia kisha maongezi yakawa yamezidi kunoga,ila mwishowe Mzee mwakipesile alimwambia Makongoro kuwa wapite shambani kwake ili akachukue maembe..kitendo ambacho kilimfrahisha sana Makongoro…asijue kuwa ile ilikuwa ni njama ya Mzee mwakipesile kumvuta Makongoro katika familia ya kichawi…hali ya kuwa Mzee mwakipesile nae asijue kuwa Makongoro tayali ameshakuwa mchawi.
“Bibi tangulia kidogo kidogo…ngoja mimi nikachume maembe kwa rafiki yangu…maana naona leo hujanibebea hata kipolo..”
Alisema Makongoro huku akizipiga hatua kuelekea kwenye shamba la mwakipesile,,wakati huo Mzee mwakipesile alikuwa tayali amesha piga hatua kadhaa za kutangulia.
“Leo lazima huyu mtoto aingie kwenye familia yetu..yaani inyeshe mvua liwake juwa lazima aitwe mwana nkulu”
Alisema hivyo Mzee mwakipesile kwa kujiamini ndani ya nafsi yake..huku wakielekea shambani..ambako huko walitokea wengine wachawi ambao walijibadilisha wakawa katika hali ya kawaida.
“Eeh niambie rafiki yangu..mbona ulipotea siku mbili hizi??..”
“Amna babu mimi mbona nipo tu. !!..
“aaah hapana bwana,ebu acha kunificha we niambie ulikua wapi.maana hata babu yako nae alipotea,,??..”
“Hahahaaa hofu yako tu ila mimi nipo siku zote”
Naam yalikuwa ni mazungumzo ya Mzee mwakipesile na Makongoro..ambapo Mzee mwakipesile alionekana kumpeleleza Makongoro ili aseme wapi alikoenda na babu yake,lakini Makongoro nae alipiga moyo konde kwa kutomwambia ukweli Mzee mwakipesile…licha ya kufaham kuwa siku moja nyuma alikuwa gambosh yeye na babu yake ambae ni Mzee baluguza.
Hatimae walifika shambani..kwa kuwa Makongoro alipinda sana maembe,hivyo alijikuta akitabasam huku kimoyomoyo akijisemea ” Hata kwa ndumba sirudi mjini..maana mjini matunda kama haya mpaka utumie pesa..” Na wakati Makongoro alipokuwa akijisemea maneno yale,punde si punde Mzee mwakipesile alisikika akisema “Rafiki panda juu angua maembe uyawezayo kisha tukae chini hapa ili tule,,au unasemaje??.” Makongoro akitabasamalijibu “sawa tu babu ila sitokaa sana kkwani natakiwa kumuwahi bibi kabla hajafika shamba..”
“aah sawa sawaa,,fanya haraka basi..”
Alijibu Mzee mwakipesile huku akiwatazama wale wachawi waliojigeza kuwa watu wa kawaida…na hapo hapo mwakipesile alitoa ishara ya kichawi,,ashara ambayo iliwafanya wale watu kujiandaa kwa kuzifunga vizuri hirizi zao.
Na mala baada Makongoro kulidhika na maembe aliyo yaangua,hatimae alitelemka kutoka juu ya mwembe..ghafla alishtuka kufika chini na kutokumwona Mzee mwakipesile..Hivyo haraka sana alipasa sauti ya kumwita lakini Mzee mwakipesile hakuitika..kitendo ambacho kilimjengea fikra Makongoro akidhania kuwa huwenda Mzee mwakipesile kaenda kujisaidia mbali na shamba lake.
Makongoro aliketi chini ya mwembe huku akiendelea kumsubili mwakipesile,,wakati huo akiendelea kula maembe hali ya kuwa macho yake yalionekana kuwa na hofu,,kwani muda wote yalikuwa yakitazama huku na kule.
Lakin baada Makongoro kukaa chini ya mwembe kwa muda wa dakika kama sita,ghafla hirizi yake aliyopewa na mkuu wa wachawi ilianza kumbana..ambapo Makongoro alikumbuka jana usiku jinsi hirizi yake ilivyombana na punde si punde akawa ametokea Mzee kinono kwa dhumuni la kutaka kumuua…Hivyo baada Makongoro kukumbuka hilo tukio,haraka sana alisimama kisha akatazama kila pande kwenye shamba lile la Mzee mwakipesile..Na punde si punde wale watu walirudi katika hali yao ya kichawi….Makongoro alishtuka baada kuwaona wachawi wale,kwa sauti Kali alimwita Mzee mwakipesile pasipo kufaham kuwa katika wachawi wale alikuwemo Mzee mwakipesile.
Na baada Makongoro kuona haitikiwi na Mzee mwakipesile,,hima alitimua mbio,cha ajabu hakuweza kuyaacha yale maembe alikimbia nayo…wakati wachawi wale nao walipoona Makongoro kakimbia,,walitazama kisha wakashikana mikono..punde si punde walipotea wakaibukia mbele ya Makongoro ambae alikuwa kasi kuwakimbia wale wachawi.
Hivyo wale wachawi wakiongozwa na Mzee mwakipesile,baada kumfikia Makongoro,,walijitwajanya kwa kumzunguka Makongoro ili waweze kumshambulia kwa pamoja..lakini kabla hawajaftua makombola yao ya kichawi ghafla Makongoro alipotea pale katikati yao kisha akaibukia sehem nyingi huku akicheka kwa dharau,,wakati huo akila embe akiwatazama .
Hakika wale wachawi baada kushuhudia kitendo kile alicho kifanya Makongoro,walipigwa na butwaa hasa Mzee mwakipesile ambae alipewa jukum na mkuu wake..jukum la kumuunganisha Makongoro katika familia ya kichawi.
“Mmh huyu nae tayali kafuata nyendo za babu yake..hivi nitamuweza kweli??..” Alijisemea Mzee mwakipesile huku akimtazama Makongoro ambae nae alikuwa bize akila embe akisubili aone watamfanya nini ili na yeye aweze kujibu mashambulizi.
“Mzee mwenzangu..mtoto huyu si wakawaida bwanaaa..mimi naona bora tukamuundie kamati ili tujuwe tutamzibiti vipi..” Alisikika mmoja ya wachawi waliokuwa wakimsaidia mwakipesile kumpata Makongoro.
“Haswaa sio Siri maana huu uchawi alionao huyu mtoto si wa nchi hii” Aliongeza kwa kusema hivyo mchawi mwingine.
Lakini licha ya Mzee mwakipesile kupewa huo ushauli na wachawi wenzake,hakutaka kulidhika mpaka amjaribu tena Makongoro..ambapo aliweza kumrushia kombola la kichawi..kombola ambalo Makongoro aliweza kulidaka kisha kulirudisha kule liliko toka..
“Unaona sasa Mzee ushalizua balaa…tatizo wewe mbishi..” Mchawi mmoja alisikika akisema hivyo kwa hasira baada kuona kombola likiwafuata..ila kabla hakijawafikia walipotea..ambapo nae Makongoro alipotea na kuibukia shambani kwa bibiyake…Na punde si punde bibi yake nae alifika..Hivyo Bi Mazoea ambae ni bibi yake Makongoro,alishangaa kumkuta Makongoro shambani hali ya kuwa Alimwacha nyuma akielekea shambani kwa Mzee mwakipesile kuangua maembe akiwa na mwenye shamba ambae ni mwakipesile.
“Mmmh wewe Makongoro..umefikaje hapa na umepitia wapi..?” Alihoji Bi Mazoea akitaka kufaham ukweli kutokakwa mmjukuu wake Makongoro.
“Bibi tufanye kwanza kazi…hayo mengine tutaongea tu..kwanza Leo sikukuu ya pasaka kwahiyo tutoke mapema ili niwahi kwenye banda la video”
“Video??..Utavionea wapi hapa kijijini??..”
“Hata kijiji cha pili mimi nitaenda tu” Alijibu Makongoro huku akiendelea kuchimba mihogo.
“Haya bwana nyie watoto wa siku hizi mnataabu sana..yaani mnaliwa hela zenu eti kisa kuwaangalia watu wasio waona wala kuwajuwa..” Bi Mazoea nae aliongeza kwa kusema hivyo,,maneno ambayo yaliweza kumfanya Makongoro kucheka.
Hivyo baada kumalizika shunghuli za shamba ..Makongoro na bibi yake walirudi nyumbani..ambapo Makongoro baada kufika alichukua ndoo kisha akaelekea kisimani kuchota maji ya kuoga ili ajiandae kwenda kijiji jirani kutazama movie.
Na baada Makongoro kujiandaa..Alipewa chakula na bibi yake..chakula ambacho kilikuwa ni Ugali na kumbikumbi walio kaangwa….ila kwa kuwa Makongoro hakukizoea kile chakula,hatimae alikula kidogo kisha akamuaga bibi yake kwa safari ya kwenda kijiji jirani kutazama movie na moja ya matembezi,,kwa maana siku hiyo ilikuwa ni sikukuu ya pasaka.
Lakini kabla Makongoro hajaanza safari yake.. Aliitwa na bibi yake..ambapo Bi Mazoea alimwambia mjukuu wake kuwa asile chakula kwenye nyumba ya mtu hatakama sikukuu..kwani licha ya asilimia kubwa ya watu wengi sikukuu hula wali na nyama..lakini hali hiyo ni tofauti katika kijiji cha bhonde..ambapo wanakijiji wa kijiji kile hula nyama za watu kutokana na asilimia kubwa ni wachawi.
Na wakati hayo yakiendelea..upande wa pili nyumbani kwa Mzee mwakipesile,,walionekana wazee wakijadili Mambo mbalimbali huku wakiwa na ndioo iliyosheheni pombe ya kienyeji.. bila kusahau pembeni walikuwa wakisikiliza muziki kwenye radio mbao iliyo chakaa kwa vumbi na nyuzi za buibui…Na katika majadiliano yale,,jambo moja kuu ni jinsi gani wataweza kumvuta Makongoro katika familia yao ya kichawi..hali ya kuwa Makongoro nae ameshakuwa mchawi??..
Kwa hakika waliumiza sana vichwa wazee wale ambao walionekana kumsaidia Mzee mwakipesile kwa namna moja ama nyingine ili aweze kumpata Makongoro.
Na wakati kila mmoja akiendelea kutafakali jinsi ya kufanya..mala ghafla Mzee mmoja alikohoa kisha akasema ..”Jamani wazee wenzangu,mimi nimepata wazo la kulinyia kazi..Na nina Hakika asilimia zote endapo tukilifanyia kazi,basi yule mtoto hatoweza kutupa shida..” Alisema hivyo yule mzee,,wakati huo wenzake wakionekana kumsikiliza kwa umakini.
“wazo gani hilo ebu tuambie mzee mwenzetu.” Alijibu Mzee mwakipesile huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kulijuwa hilo wazo…ambapo yule Mzee aliesema kuwa ana wazo,alikunywa pombe kidogo iliyokuwa kwenye kikombe kikubwa..kisha akasema…
“Jamani huyu mtoto kama mnavyo muona,,uchawi wake unatisha sio mchezo…Hivyo mimi nilikuwa napendekeza kwamba hakuna haja ya kumuunganisha kwenye familia yetu..maana uchawi alionao tu unamtosha..” Mzee yule kabla hajaendelea kutoa wazo lake,ghafla Mzee mwingine alidakia akisema..”Sasa unaongea pumba gani we Mzee..eeh au kuzeeka kwako na akili pia imezeeka??….Haya tusimuunganishe kwenye familia yetu halafu tumfanye nini sasa” Alidakia huyo Mzee akisema maneno hayo kwa hasira kali,,ambapo yule Mzee aliekua akitoa wazo lake alionekana kuwa mpole huku akimsikiliza Mzee mwenzake kile anacho kiongea kwa hasira.
Hivyo mala baada Mzee yule kumaliza kuongea kwa hasira akipinga wazo la mwenzake,hatimae alikaa kimya,,kisha yule aliekatishwe nae alisikika akisema “Tatizo wewe mwongeaji sana,,istoshe unafoka kama vile unaongea na watoto wako….Sasa kwa taarifa yako hiyo mipango yenu muifanye wenyewe mimi simo kwa kazi hii ni ya mwakipesile”
Kwisha kusema hivyo yule Mzee alinyanyuka kutoka kwenye kigoda chake..kisha akarudi nyumbani kwake huku akiongea njia nzima.
Hivyo baada yule Mzee kuondoka..wale wazee walio salia wote kwa pamoja walikubaliana kummaliza yule Mzee mwenzao,,ambae aliitwa mzee chande..kwani waliamua kufanya vile baada kuonekana kuwa Mzee chande huwenda akawa msaliti juu yao.
“Mizee mingine bwana..yaani sisi tunakaa makini kumsikiliza kumbe anacho kiongea chenyewe hata hakieleweki..eti zee lote lile miaka dahali lipo kwenye uchawi ..halafu Leo hii anamwogopa mtoto mdogo kama yule..??..” aliongea maneno hayo Mzee mwakipesile..maneno ambayo yaliwafanya wazee wenzake kuachia cheko kubwa huku wakinywa pombe yao iliyokuwa kwenye ndioo kubwa..Na kwa mbali wakisikiliza muziki kwenye radio mbao.
Baada wazee wale kumaliza kunywa pombe yao..hatimae waliagana lakini kabla hawajasambaa,,Mzee mwakipesile aliwakumbusha kuhusu suala la kumuuwa Mzee chande ambae alionyesha usaliti..ambapo wazee wale walitii na kisha wakakubalina wakutane saa tano usiku sehem malum ili wajue namna gani wataweza kumuuwa Mzee chande msaliti.
Wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako alionekana Makongoro akizipiga hatua kuelekea kijiji jirani kwenda kutazama movie…lakini wakati Makongoro alipokuwa akitembea hana hili wala lile..mala ghafla nyuma yake alitokea Sudi mtoto wa Mzee kinono…Sudi akiwa katika mavazi yake ya kichawi,alizipiga hatua kumfuata Makongoro..Na kabla hajamfikia,Sudi alimrushia kombola Makongoro..hali ya kuwa Makongoro nae hirizi yake aliyopewa na mkuu wa wachawi gambosh ilianza kumbana,,na hapo hapo alijuwa tayali kuna tatizo hivyo kwa kuhusi tu lipotea ndani ya nusu sekunde kisha akaonekana tena live…na lile kombola la kichawi alilorusha Sudi likawa halijampata.
Makongoro aligeuka nyuma akamwona kijana mdogo mwenye makamo kama yake akiwa katika mavazi ya kichawi…Hakika Makongoro alijikuta akicheka huku akiendelea na safari yake ya kuelekea kijiji jirani.
Lakin licha ya Makongoro kumpotezea Sudi kijana wa Mzee kinono..ila Sudi bado aliendelea kumchokoza Makongoro..akasahau onyo aliyopewa na baba yake kuhusu Makongoro mjukuu wa Mzee baluguza…Na hapo ndipo Makongoro uvumilivu ulipo mshinda,hivyo kwa kutumia mkono wake uliokuwa na hirizi alimnyooshea kidole Sudi,,na punde si punde Katika kidole chake Makongoro ulitokea moto mwembamba,moto ambao ulikwenda kumpata Sudi..haikupita dakika Sudi alidondoka chini akafa.
Baada Sudi kupoteza maisha..Makongoro aliogopa sana hivyo aliamua kuahilisha safari yake akawa amerudi nyumbani..moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani kwake huku akionekana kuwa na hofu juu ya kile alicho kifanya..
Lakini kitendo kile cha Makongoro kupitiliza hadi chumbani kwake bila kumsalimia bibi yake ambae alikuwa sebleni akipika chakula cha usiku..kiliweza kumshtua Bi Mazoea bibi yake Makongoro..ambapo aliweza kumeita ili amwambie kilicho msibu,,ile Makongoro hakuitikia…Na wakati huo huo Mzee baluguza nae alifika nyumbani,hivyo ikabidi Bi Mazoea kumwambia mume wake akamuulize kinacho msibu Makongoro.
Mzee baluguza baada kuambiwa vile..haraka sana alizipiga hatua kuelekea chumbani kwa Makongoro..kwa sauti ya kunong’ona Mzee baluguza alimuuliza mjukuu wake kitu kinacho msumbua.
“Babu nimezusha balaa..kumbe uchawiwenu unauwa kabisa..”
Alisikika ikisema hivyo Makongoro huku kilio kifuatia,,na Mzee baluguza baada kuona hali ile,,hima aliongea maneno yake ya kirugha huku akisugua kiganja chake…Na punde si punde kwenye kiganja chake walionekana wachawi wa kijiji kile cha bhonde wakiwa wamekusanyika kwa nia kumtaka Makongoro na kisha kumuuwa Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro.
“unaona sasa mjukuu wangu??..Kwahiyo kaa ukijuwa kuwa tumezungukwa na madui wengi..Na kauli mbiyu yetu ni dawa ya moto maji..Na sio dawa ya moto moto..hahahaaaaa wao wanawasha halafu sisi tunazima..futa machozi mjukuu wangu hujakosea kumuuwa yule mtoto wa Mzee kinono kwani ukiona hivyo nae alikuwa akikuwinda ili akuue..” Alisema hivyo Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake,,hali iliyomfanya Makongoro kujiamini juu ya kile alicho kifanya.
Na giza lilipo tanda katika kijiji kile cha bhonde…Mzee mwakipesile alipanda ungo wake na kisha kutua sehem ile waliyoahidina wakutane na wazee wenzake.Hivyo punde si punde wale wazee nao walitua,ambapo walikubaliana kwenda kumuuwa Mzee chande kisha waelekee tena kwa Makongoro kwenda kujaribu tena bahati yao.
Kumbe wakati wazee wale walipokuwa wakipanga mikakati ya kumuua Mzee chande..Mzee chande nae machale yalimcheza,ambapo alichukua ungo na kibuyu chake kidogo..kisha akapaa kuelekea Congo ili kuongeza uchawi zaidi wa kuweza kujirinda dhidi ya Mzee mwakipesile na wenzake ambao wamepanga kumuuwa kabisa.
Hivyo wakati anaiacha ardhi na kuliona anga tu..mwakipesile na wenzake nao walitua nyumbani kwa kwake chande,,ambapo walijikuta wamechelewa kumuwahi Mzee chande.
Hakika roho ilimuma sana Mzee mwakipesile ambae ndio alikuwa kiongozi wa msako..Lakini yote kwa yote aliwataka wazee wenzake waelekee nyumbani kwa Mzee baluguza kwenda kumfuata Makongoro..hali ya kuwa Makongoro nae ameshaambiwa kuwa amezungukwa na maadui,,hivyo kuuwa ni jukum lake.
Kikao cha muda mfupi walikaaa Mzee mwakipesile na wachawi wenzake watatu…ambapo Mzee mwakipesile alisikika akisema. “Jamani kwa kuwa tumemkosa huyu mzee chande,,sasa safari hii tuelekee kwa Mzee baluguza,kwenda kumfuata mjukuu wake..lakini napenda kukumbusha kuwa tuwe tayali kwa mapigano maana nadhani kila mmoja hapa Kati yetu ameweza kushuhudia uwezo wa yule mtoto..je,kweli si kweli??..”
“Kweli kabisa..” waliitikia wale wachawi wengine baada Mzee mwakipesile kusema maneno hayo akiwaasa wenzake wawe makini pindi watakapo elekea nyumbani kwa Mzee baluguza.
Na mala baada kuelewana,,Mzee mwakipesile na wachawi wenzake walijifunga vizuri hirizi zao,kisha wakanywa damu ya binadam iliyokuwa kwenye kibuyu chao…Na hapo hapo safari ya kwenda kwa Mzee baluguza ilianza,,ambapo walipaa angani kwa kutumia ungo.
ITAENDELEA
Sehemu Ya Tano (5)
Lakin wakati wachawi wale walipokuwa angani wakielekea kwa Mzee baluguza kumfuata Makongoro,,upande mwingine nako alionekana Mzee baluguza akizipiga hatua kuelekea chumbani kwa Makongoro,,na mala baada kufika aliamwamsha mjukuu wake,,kisha akamwambia ajiandae ili waelekee kwa rafiki yake Mzee baluguza kwenda kula chakula alicho alikwa usiku huo wa pasaka.
Makongoro baada kuamshwa na babu yake,,hima alijiandaa kwa kuvaa mavazi yake ya kichawi na kujifunga hirizi yake mkononi,,na punde si punde alipotea mle chumbani kwake,akatokea nje ambapo kwa kutumia mkono wake uliokuwa na hirizi aliyopewa na mkuu wa wachawi..aliunyoosha juu,ghafla ukatokea ungo mweusi…aliushusha chini kisha akaketi ndani ya ule ungo..wakati huo huo Mzee baluguza nae akitokea nje akiwa mkononi ameshikilia vibuyu viwili ila kimoja alimkabidhi Makongoro na kingine alibaki nacho.
“Kunywa kwanza hiyo damu kisha tuanze safari..” Alisema Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake…ambapo Makongoro aliichekecha kwanza ile damu iliyokuwa ndani ya kibuyu kisha akanywa kidogo tu.
Na baada Makongoro kunywa ile damu,Mzee baluguza alisikika akisema tena. “Safari inaanza sasa mjukuu wangu..cha kuzingatia ni kuwa makini angani kwa maana anga zingine hazifai..”
“Sawa babu nimekuelewa..” Alijibu Makongoro..Na punde si punde walipaa angani babu na mjukuu kila mmoja akiwa na ungo wake.
Hivyo kitendo kile cha Mzee baluguza na Makongoro kupaa angani..ghafla akitua Mzee mwakipesile akiwa na wachawi wenzake,,ambapo Mzee mwakipesile alikasirika sana baada kukuta Makongoro kaondoka..akajikuta akiishiwa nguvu,wakati huo akiwa amebakiza siku mbili tu kati ya zile alizopewa na mkuu wake..siku za kumfuata Makongoro katika familia ya kichawi..Na endapo kama ikatokea Mzee mwakipesile kashindwa jukum hilo,moja kwa moja atagezwa kuwa kitoweo cha misukule.
Hali ya kuwa yakiendelea hayo..gambosh nako Mambo yalizidi kumwendea kombo kwa mchawi albino,Kwan baada kukatwa kiungo kimoja kimoja kwenye mwili wake na mtoto mdogo wa kichawi ..mwishowe alipoteza maisha..Hivyo kwa kutumia damu yake na viungo vya sehem ya Siri,,watumishi wa gamgambosh waliweza kupata dawa ambayo iliweza kuirudisha misukule iliyokuwa imetoroka..Hakika hapo ndipo gwimo alipopata nafasi ya kussmehewa kwa maana yeye hakuwa mbishi kama ilivyokuwa kwa mchawi albino ambae alijiamini kwa kila kitu.
Hivyo baada gwimo kusamehewa..hatimae aliambiwa afumbe macho,,na ndani ya dakika kadhaa aliambiwa afumbue,,gwimo alishangaa kujikuta Tanzania ndani ya dakika kadhaa..alijisemea “Ama kweli duniani kuna uchawi..yaani mimi usafiri wangu ungo kumbe kuna usafiri mwingine wa haraka haraka tu??!!..” Alijisemea hivyo gwimo huku akizipiga hatua kuelekea nyumbani kwake…Na baada kufika alitaharuki kuona watu wengi nyumbani kwake na maturubai mbili mbili,,ambapo gwimo Alizidi kupigwa na butwaa baada kuwaona watu wakimkimbia,,huku baadhi yao wakisema “Gwimo kafufuka..Jamani gwimo hajafa..”
“Sijafa??…Kwahiyo walijua mimi nimekufa..??..” Alijiuliza gwimo baada kusikia zile sauti zilizokuwa zikimwongelea yeye kuhusu suala la kufa..
Kwingineko kijijini bhonde..wazee wa kijiji walikaa kikao cha usiku kwa usiku..wakipanga kumuuwa Mzee baluguza kwa njia yoyote baada kubainika kuwa yeye Mzee baluguza ndio alimuuwa mama chiku kwa kumkata shingo…ambapo mwisho waliafiki hilo suala watalifanyia kazi kwa kumpa hiyo kazi mchawi Kati ya wachawi ambae anaitwa Mzee kaje..Mzee ambae alikuwa na kila aina ya uchawi.
Kwa hakika wazo lile la kumpa kazi Mzee kaje ili ammalize Mzee baluguza..liliwafurahisha wazee wale wa kijiji..ghafla walijikuta wakimmwagia sifa nyingi Mzee kaje huku wakiamini kuwa Mzee baluguza kiboko yake ni Kaje pekee.
Lakini baada wazee hao kupata suluhisho,Hatimae Mzee kinono nae alirejea kutoka mindu alikokuwa ameenda kuongeza uchawi ili aweze kumkomesha Makongoro..Na kitu kibaya zaidi alikupofika nyumbani kwake hakumkuta mwanae…Hivyo haraka sana alifanya uchawi wake,,ambapo alishtuka kumwona mwanae akiwa amefariki,,hivyo alitaka kujuwa mtu alie muuwa moto wake..punde sio punde akaonekana Makongoro ndio muuaji…Na vyote hivyo Mzee kinono alivitazamia kwenye TV yake asilia.
“Sasa huyu mtoto kavuka mpaka,,kiukweli sitomwacha Salama hata akikimbilia kwao mjini nitamfuata..” Kwa majonzi Mzee kinono akiomboleza kifo cha mwanae kipenzi kijana Sudi..aliapa hivyo huku akitamani itokee siku yoyote akatunae live na Makongoro mjukuu wa Mzee baluguza.
Mzee kinono alilaani kitendo kile alichokifanya Makongoro kwa mwanae..Hivyo alitamani siku yoyote akutane na Makongoro ili alipize kisasi kwa kumuuwa kabisa kama yeye Makongoro alivyofanya kwa mwanae.
Na wakati mzee kinono akitamani siku hiyo itokee,upande mwingine nako Mzee baluguza akiwa na mjukuu wake angani,ghafla walijikuta wakiweweseka.. lakini kwa uzoefu na umahili aliokuwa nao Mzee baluguza,aliweza kumwondoa hofu mjukuu wake hadi pale walipofanikiwa kuchomoka kwenye ile dharuba..ambapo walifanikiwa kutua Salama nyumbani kwa rafiki yake ambae nae alikuwa mchawi kama ilivyo kwa Mzee baluguza.
Baada Mzee baluguza pamoja na Makongoro kutua Salama,walipokelewa na wenyeji wao,,kisha mazungumzo kadhaa yalifuatia..ambapo muda wa chakula ulipo wadia,Mzee baluguza na mjukuu wake walikula na kunywa.Chakula chao ambacho ni nyama ya binadam huku kinywaji ikiwa damu .
kwa kuwa Makongoro alikuwa amesha zoea kile chakula,hivyo hakupata tabu alikula bila kuwa na mashaka yoyote.
Hali ya kuwa kijini bhonde..wachawi wote walijikusanya maeneo yao yale yale,agenda yao ikiwa ni kumwondoa duniani Mzee baluguza baada kugundulika kuwa kweli yeye ndio aliemuua mama chiku..Lakini wakati hiyo agenda ilipokuwa ikizungumziwa ,ghafla alinyoosha mkono mzee mmoja,ambapo baada kupewa nafasi alikohoa kidogo kisha akasema. “Jamani wananzengo,,mimi sioni sababu ya kuumiza kichwa kwa huyu mtu mmoja..japo ni kweli Mzee baluguza anatusumbua,lakini kiboko yake yupo..” kwisha kusema hivyo,yule mzee alinyamanza kidogo huku akionekana kusugua kiganja chake na punde si punde kwenye kile kiganja alitokea mchawi Kaje.
“Nani asiemjuwa huyu mtu..??..” Alisema yule Mzee aliepewa nafasi ya a kuongea mbele ya jopo la wachawi..wakati huo akihoji hivyo muda wote mkono ule wenye picha ya Kaje ulikuwa juu juu akiwaonyesha wenzake..kitendo ambacho kiliweza kuwafurahisha wachawi wote baada kuiona picha ya Kaje,ambapo vegelegele kutoka kwa wachawi wa kike vilisikia,huku mirunzi nayo kwa upande wa wanaume napo vilisikika vilivyo…na punde tu sifa za kumsifia Kaje zilifuatia,kitu ambacho kiliweza kuzua fujo maeneo yale ambapo mkuu wa wachawi wa kijiji cha bhonde Bi kileleganya aliweza kuzituliza zile fujo..Na kisha akafunga Mkutano Kwan alichotaka wakijidili namna ya kukudhibiti,kimejibiwa haraka Hivyo hakuwa na haja ya kuendelea na Mkutano…
Hivyo Bi kileleganya alipotea,haikuchukuwa muda wale wachawi wengine nao walianza kupotea mmmoja baada ya mwingine huku wakionekana kuwa na furaha wakiamini kuwa Mzee Kaje anaweza kumzima Mzee baluguza bila wasiwasi wowote.
Na baada wachawi wale kupotea mkutanoni,upande wa pili alionekana Mzee baluguza akiwa na mjukuu wake angani ndani ya ungo lasmi wakirejea nyumbani.
Safari hiyo hawakupata misuko suko yoyote,walitufanikiwa kutua Salama nyumbani kwao.
Kesho yake asubuhi asubuhi mapema,kama ilivyokawaida kwa Mzee baluguza kwenda kukagua mitego yake kama imefanikiwa kunasa mnyama au lah,wakati huo Makongoro na bibi yake waliekea shamba kufanya kazi mbali mbali za shamba.lakini Makongoro na bibi yake kabla hawajafika shambani,ghafla nyuma yao alitokea Mzee kinono akiwa katika mavazi yake ya kichawi,,ambapo Mzee kinono alionekana kuwa na hasira kali haraka sana aliutumia uchawi wake aliotoka nao mindu kwa kurusha makombola mawili,,kombola moja likamlenga Makongoro na lingine likamlenga bibi yake Makongoro..wakati huo Makongoro nae alikuwa Tayali ameshahisi nyuma yake kuna hatari,hima aligeuka na akaweza kuyazuia yale makombola ya Mzee kinono…Na hapo ndipo Bi Mazoea alipo shuhudia uwezo wa mjukuu wake akajikuta uchawi alionao yeye na uchawi alionao Makongoro,uchawi wa Makongoro ni moto wa kuotea mbali.
Mzee kinono baada alishangaa kuona Makongoro kafanikiwa kuyazuia yale makombola,lakini kwa kuwa utu uzima dawa,hatimae Mzee kinono hakutaka kuonyesha udhaifu kwa mala ya pili mbele ya Makongoro na hapo ndipo alipo anza kurusha makombola kumi mfurulizo ambapo kombola moja tu ndilo lililo fanikiwa kumpata Makongoro,,Makongoro akawa ameanguka chini huku akipiga kelele.
Na hapo Bi Mazoea hakufurahishwa na kitendo kile cha mjukuu wake kupigwa na Mzee kinono,hivyo nae alijiandaa kichawi kisha akapana na Mzee kinono ambae alionekana kuwa na uchawi makali kiasi kwamba hata Bi Mazoea nae alichemka kumdhibiti Mzee kinono..
lakini baada Makongoro kutulia chini ndani ya dakika kadhaa akiugulia maumivu,punde si punde alinyanyuka tena akiwa na nguvu mpya na hali mpya,ambapo kwa kutumia mkono wake uliokuwa na hirizi aliyopewa na mkuu wa wachawi alimpush Mzee kinono,,,hakika kinono nae aliweweseka na kabla hajaanguka chini…..Makongoro alimwongezea kombola la kichawi lilofanikiwa kumpata Mzee kinono kichwani,,papo hapo Mzee kinono akawa amepoteza maisha.
Hali ya kuwa bibi yake Makongoro nae hali yake vile vile hakuwa nzuri kwa maana alipo pigana na Mzee kinono alijeruhiwa sehem ya mwili wake..Na hivyo safari ya kuelekea shambani ikawa imekomea hapo,ambapo Makongoro alichuchumaa chini huku akiwa amemgusa bibi yake,punde si punde alipotea akaibukia nyumbani kwao,,ambapo nako alukuta nyumba imechomwa moto na wanakijiji..kitendo ambacho kilimuumiza Makongoro…akajikuta hana la kufanya zaidi ya kudondosha machozi ya hasira..wakati huo huo Mzee baluguza nae alirudi kutoka kikagulia mitego yake,nae alipigwa na bumbuwazi baad kukutana nyumba yake ikiwa imeteketea na moto huku upande mwingine akimwona mke wake yupo hoi bitaabani.
Kwa Hakika Mzee baluguza alilia sana kwa uchungu,kwani baadhi ya vitu vyake vya kichawi viliteketea na moto…Lakini kilio chake kilikatika baada kumwona mtu akizipiga hatua kuelekea kule alipokuwa yeye,,mtu huyo mkononi alikuwa na bahasha ambapo baada kumfikia Mzee baluguza alimsalia kisha akamkabidhi bahasha.
Hivyo kwa kuwa Mzee baluguza alikuwa hajui kusoma,moja kwa moja alimkabidhi Makongoro ile bahasha,ambapo Makongoro baada kuifungua alikutana na ujumbe kuwa anahitajika arudi mjini ili akaendelea na masomo ya secondary kwa sababu kafanikiwa kufauru..Na kizuri zaidi katika barua ilieleza kuwa Makongoro aende mjini na babu pamoja na bibi yake ili uzee wao wakaumalizie mjini.
Habari ambayo ilipo mfikia Mzee baluguza alifurahi sana haraka sana alikwenda kijiji cha pili kutafuta mteja wa kumuuzia shamba ili apate nauli ya kuondokea…alifanikiwa kumpata japo aliliuza shamba lake kwa bei ya hasara lakini nauli ya kumfikisha mjini ilitosha..zaidi alimpatia mke wake dawa za miti shamba ili arudi katika hali yake..kweli ndani ya masaa mawili matatu Bi Mazoea alipata ahueni,hivyo saa kumi na mbili ilipofika Safari ya kuelekea stendi ya gari ya haisi ziendazo mjini ilianza,ambapo kabla ya kufika stendi Makongoro na babu yake pamoja na Bibi yake walivua hirizi zao na kisha kuzitupa..nazo hirizi hizo zilipo angukia zilipotea kimiujiza.
Usiku ulipo ingia,Mzee mwakipesile alijikuta akiwa katika wakati mgumu,baada kushindwa kufanya kile alicho tumwa na mkuu wake..ambae alimpa kazi mwakipesile kazi ya kumuunganisha Makongoro kwenye familia yao ya kichawi…
Hakika Mzee mwakipesile alilia sana,hivyo akaon kuliko akawe chakula cha misukule,heri ajiue mwenye kwa kula nyongo ya paka ya paka wake.
Mzee mwakipesile akawa amekufa kifo cha namna hiyo…huku mzee chande msaliti nae alirejea kutoka nchi Congo alikokwenda kusaka uchawi wa kujilinda dhidi ya maadui zake,lakini Chande alijikuta akikosa vyote kwa maana siku zote uchawi huwa hauvuki maji…..Kitendo kile cha Chande kuukosa uchawi,hakuwa na namna zaidi aligeukua kumkumbuka mungu wake huku akitubu juu ya yale aliyo yafanya pindi alipokuwa mchawi..Na yote hayo hakuyafanyia pale bali aliyafanya baada kukihama kijiji kile cha wachawi.
Usiku uleule..Mzee Kaje alitua ndani ya kile kijiji,kwa niaba ya kupigana na Mzee baluguza,,lakini Kaje pamoja na wanakijiji wote kwa pamoja walijikuta wakitaharuki baada kusikia kuwa Mzee baluguza akaondoka na mjukuu wake mjini kwa mwanae…kitendo ambacho kilimfanya baadhi yao kujisikia furaha kuondoka kwa Mzee baluguza,huku wengine wakitamani auliwe kabisa ili asionekane duniani.
Wakati huo tayali Mzee baluguza na mke wake pamoja na Makongoro,tayali walikuwa wameshakata ticket ya bus liendolo Dar es salaam..Hivyo walilala pale pale stendi ya mkoa hadi asubuhi ambapo safari ilianza huku lasmi Mzee baluguza na Bi Mazoea pamoja na Makongoro wakikiacha KIJIJI CHA WACHAWI na kuelekea zao mjini huku wakiwa hawana hata lepe la uchawi wala hirizi.
Na hata walipo fika dar es salaam.Makongoro alikuta habari kuwa mwalimu shija ambae alimwona gambosh kafariki baada kuutwa na tuhuma za kichawi,,ambapo alipigwa hadi na wananchi wenye hasira kali.
BAADA WIKI TATU..3
“Mmmh ila mjukuu wangu ulikuwa na nyota ya kuwa mchawi??..” Alisema Mzee baluguza akimtania mjukuu wake huku wakiwa sebleni wawili tu wakitazama video saa za jioni.
“Daaa we acha tu..ila nime miss nyama za ndezi babu..au turudi zetu kijijini..” Akitabasam Makongoro alijibu hivyo..kitendo ambacho wote kwa pamoja wakacheka huku Mzee baluguza akisema..
“Weeee kama unauchawi wako mpya basi rudi..tofauti na hivyo utanyonyolewa hadi ufe..Hahahaaa” Alisema hivyo Mzee baluguza,na mwisho wa yote alimaliza kwa kusema.
“Mjukuu wangu uchawi hauna maana hukupi maendeleo yoyote..Hakika huu ni wakati wa kumrudia mungu wetu ili atusamehe makosa yetu”
MWISHO